Maelfu waandamana Madrid kuiga Ugiriki - LEKULE

Breaking

31 Jan 2015

Maelfu waandamana Madrid kuiga Ugiriki


 Barabara kuu za Madrid zimajaa maelfu ya watu wanaofanya mhadhara kuunga mkono chama cha mrengo wa kushoto cha Uspania, Podemos, kinachopinga sera za kubana matumizi.

Waratibu wanasema hayo ni maandamano ya kutaka mabadiliko.

Ni maandamano makubwa kabisa ya Podemus ambayo yamepata nguvu baada ya ushindi wa chama cha Syriza nchini Ugiriki.

Waandamanaji walipepea bendera za Ugiriki na kupiga kelele dhidi ya wanasiasa wa sasa wa Uspania.

Podemos ilianza mwaka jana na sasa inaongoza katika kura za maoni, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwisho wa mwaka.

No comments: