Kadhim Jalali, Mbunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran 'Bunge la Iran' ambaye yuko safari nchini Uturuki kwenye ujumbe wa Iran unaoshiriki kwenye kikao cha Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu amesema kuwa, kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu ni mstari mwekundu kwa nchi za Kiislamu. Kadhim Jalali ameyasema hayo pambizoni mwa kikao hicho mjini Istanbul na kusisitiza kwamba, Maspika wa Muungano wa Mabunge ya Kiislamu licha ya kulaani vikali kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu, wametaka yaendelezwe mapambano dhidi ya ugaidi na hasa ugaidi wa kiserikali unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Jalali ameongeza kuwa, Maspika wa Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu wameziunga mkono kikamilifu nchi zinazotaka kujipatia teknolojia ya nyukllia kwa malengo ya amani. Viongozi hao pia wamesisitiza kuwa kuna udharura wa kukabiliana na njama zinazofanywa na utawala wa Israel za kueneza hofu juu ya Uislamu. Kikao hicho kilichoanza jana nchini Uturuki, kitamaliza shughuli zake leo. Dakta Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran anahudhuria kikao hicho.
No comments:
Post a Comment