Kiwanja cha ndege na bandari katika mji wa Aden nchini Yemen vimeanza shughuli zake siku moja baada ya Rais wa nchi hiyo Abdu Rabu Mansour Hadi kufikia mapatano na wapiganaji wa Kihouthi. Maafisa wa Yemen wamechukua uamuzi wa kufungua bandari na kiwanga cha ndege katika mji wa Aden siku moja baada ya Rais Hadi na wapiganaji wa Ansarullah kufikia mapatano yenye lengo la kuhitimisha mivutano nchini humo.
Maafisa usalama wa Yemen Jumatano iliyopita walifunga njia zote za kuingilia katika mji huo wa bandari wa kusini mwa Yemen kufuatia mapigano ya siku kadhaa kati ya wapiganaji wa Ansarullah na vikosi vya serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a. Mapema wiki hii pia wapiganaji wa Ansarullah waliizunguka Ikulu ya Rais huko Sana'a na kuzingira makao ya kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment