Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ni nchi ya nne kwa uwezo wa makombora duniani. Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema Iran ina hadhi inayokubalika kati ya nchi zenye uwezo wa makombora ikiwa inashika nafasi ya nne baada ya Marekani, Russia na China. Brigedia Jenerali Dehqan ameongeza kuwa Iran imeongeza uwezo wa masafa wa makombora yake kwa kuzingatia vitisho vinavyoweza kuikabili. Kwa miaka kadhaa iliyopita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta yake ya ulinzi kwa kufikia kiwango cha kujitosheleza katika uzalishaji zana na mifumo muhimu ya kiulinzi na kijeshi na kuongeza ufanisi wa kujiweka tayari vikosi vyake kwa kufanya maneva kadhaa. Pamoja na hayo, Iran imeshatoa hakikisho mara kadha kwa kadha kwa mataifa mengine hususan nchi jirani za eneo kwamba uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi nyengine na kusisitiza kuwa kanuni yake ya ulinzi inalenga kuzuia uchokozi wa adui tu. Waziri wa Ulinzi wa Iran ameashiria pia hatua ya Marekani na waitifaki wake ya kujaribu kuliingiza suala la uwezo wa makombora ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia kati ya Tehran na nchi zinazounda kundi la 5+1 na kusisitiza kwamba mazungumzo hayo yanahusu kadhia ya nyuklia tu…/
27 Dec 2014
New
Iran ni ya nne kwa uwezo wa makombora duniani
About SOSTENES LEKULE JR
Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
MAKALA
Tags
MAKALA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment