Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ameukosoa utendaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kubainisha kwamba, mahakama hiyo haina uadilifu. Desalegn amesema kwamba, mahakama hiyo haitekelezi majukumu yake kama inavyotakiwa. Waziri Mkuu wa Ethiopia amesisitiza kuwa, nchi yake inaunga mkono suala la nchi zote za Kiafrika kujitoa katika mahakama ya ICC. Ameongeza kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ni wenzo wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwamba, nchi hizo zenyewe sio wanachama wa ICC na zimekuwa zikifanya njama za kuitumia taasisi hiyo kama wenzo wa kufikia malengo yao ikiwa ni pamoja na kuitumia taasisi hiyo kuzishinikiza nchi nyingine. Waziri Mkuu wa Ethiopia amebainisha wazi kwamba, nchi yake sio mwanachama wa ICC na katu haitatia saini mkataba wa Roma wa kujiunga na mahakama hiyo kwani taasisi hiyo haina uadilifu. Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inatuhumiwa kwamba imekuwa ikiwaandama viongozi wa Afrika na kuwanyamazia kimya watenda jinai wa maeneo mengine ya dunia hususan Ulaya na Marekani. Viongozi mbalimbali wa Kiafrika wamekuwa wakikosoa utendaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na hata kuilaumu kwamba, imekuwa ikiwafuatilia viongozi wa bara la Afrika tu. Hata nchi ambazo ni wanachama wa ICC zimekuwa zikitishia kujitoa katika mkataba uliounda mahakama hiyo.
27 Dec 2014
New
Ethiopia: Mahakama ya Jinai ya ICC haina uadilifu
About SOSTENES LEKULE JR
Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
f
Tags
f
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment