Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu
162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo
cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini
Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za
kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
No comments:
Post a Comment