Sheikh Farid Had Ahmed alipotumia katiba ya Zanzibar kupinga muungan uvunjwe.Lakini jambo muhimu ni diplomasia ni usikivu na kupokea changamoto zinazotolewa kwa wapinga muuungano.Pamoja na dosari za hapa na pale,bado tunayohaki ya kujadili hivyo Sheikh Farid Had Ahmed,ambae ni msemaji wa jumuiya ya UAMSHO anaweza kuwa mtu muhimu sana katika majdiliano.Pia jeshi letu la polisi linapaswa kutumia diplomasia katika kanuni zao.Pia katika bunge tutakuwa na bunge la jamhuri ya muungano ambalo litajumuisha wabunge wa muuungano.Kusema baraza la wawakilishi la Zanzibar na Tanganyika sio serkali za maeneo hayo,bali watendaji wa kila siku wa shughuli za serikali watokanao na serikali kuu(muungano).Kwa hiyo serikali ya muungano ndio itakuwa serikali kuu na msimamizi wa shughulizote za jamhuri ya muungano;masuala ya nje,masuala ya ndani,ulinzi na usalama na makubaliano mengine kama ilivyokuwa awali na nyongeza(viambatanisho).
ZANZIBAR ILIVYOUNDA JUMUIYA YA UAMSHO.
Kuna habari nyingi sana za kuanzishwa kwa Jumuiya ya UAMSHO.Nasema maswali yaliyozoeleka sababu sio ya kwanza na hayatakuwa ya mwisho.Bahati mbaya maswali kuhusu muungano yanaambatana na harakati za uovu.Na uovu unatokana na utumwa wa mwanadamu kuhusu dini.Utumwa ambao umefika mahali uhalisia wa mwanadamu unaondoka hivyo tumefikia mahali kuunda vikundi mbalimbali kwa lengo la kupambana dhidi ya wasiokuwa waamini wa dini nyingine.Watu wa namna hii wameundwa katika nafasi mbalimbali,pamoja na kupelekwa shuleni na kusoma mambo mengi lakini hawajaelimika na wala hawakuelewa hata kipamde cha habari.Kwa namna moja ma nyingine wazanzibar wengine watasema hawakujua chochote kuhusu harakati za jumuiya ya UAMSHO.Watajitetea kuwa hawakujua wamejikuta wakijua sasa,lakini ukichunguza historia inatueleza wazi kuwa uamsho ni matokeo ya kupandwa mimba ya chokochoko kuhusu muungano pasipo hoja.Mimba ya chokochoko imezaa watoto wengi,mmojawapo ni UAMSHO.Kwa hiyo,tunachokilalamikia sasa ni matokeo tu.Kwa tukio la karibuni chini ya utawala wa Dr.Salmini Amour za Zanzibar(1995-2000).Kuna mambo mawili;Kwanza kunuia kubadili katiba ya kuendelea kukaa madarakani.Pili kujiunga na OIC hili linachekesha kama Commonwealth).Wakati wa utawala wa Dr.Salmini Amour tuliona harakati za Zanzibar kujiunga na OIC.Hiyo ni mimba mojawapo iliyozaa Uamsho.Mgongano ule ulisababisha malumbano makali kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibay(SMZ)na serikali ya Muungano.Baadae iliamriwa kwamba Zanzibar ijiondoe kwenye jumuiya ya OIC,hivyo Dr.Salmini alitimiza hilo kwa shingo upande maana aliingiza Zanzibar kwa makusudi.Katika kundi lile Dr.Gharib Bilal makamu wa raisi wa sasa alikuwa miongoni mwa wafuasi wa Dr.Salmini Amour kisiasa.Je? aliondoka kwenye mtandao wa Amour.Wengine ni Hassan Nasoro Moyo,Mohamed Seiph Hatibu,Seif Bakari,Ali Mzee,Hafidh Seleman,Brigedia Ramadhan Hadji,Brigedia Hamis Hemed,na Aboud Twalib.Aidha hayati Abeid Amani Karume alipanda mbegu kwa kufananisha muungano na koti linalobana.Pia ni mimba iliyozaa uamsho.Mimba nyingine ni wabunge 55(G55)walionyukana na Mwalimu Nyerere kudai serikali ya Tanganyika.Nao wanahusika kuzalisha uamsho.Naam......polepole ajenda hiyo imekuwa sehemu ya madai ya uamsho,kwamba lazima Zanzibar iwe mwanachama wa OIC,kisa misaada.Ni njaa na uchumi wa kutembeza bakuli.Kufilisika kwa mawazo Raisi Joachim Chissano akaitumbukiza Msumbiji huko OIC kama ilivyo kule Commonwealth.Ni kama ulemavu wa wataawala wengi wa Africa na wananchi wameiga,wamekula yamini ni omba omba tu.Hata kwenye Commonwealth ambako sasa kunatolewa masharti ya ndoa za jinsia moja kuwa kigezo cha kupewa misaada.Ndio maana Raisi Joyce Banda wa Malawi amejionyesha wazi alivyofilisika mawazo kuruhusu ushoga pindi atakapofuta sheria za kuzuia ushoga,anafikiria misaada tu.Uchumi wa kuomba omba ni ulemavu mkubwa.Sisemi kuwa Zanzibar isijiunge OIC,bali ni kichekesho kichungu waafrica wenye akili timamu wanalia na kusaga meno,kisa kupewa misaada,kuomba omba.Watumwa sugu wanaendelea kuzalishwa katika kaya zetu,kwa mahubiri ya misaada,misaada,tutasaidiwa.Hivi nyie wenzetu ni viwete hadi msaidiwe tu?.Hatuna aibu kushikiana mapanga,kisa kusaidiwa na wakoloni wa oman?.Si ndio yale yale ya Commonwealth?.Au ndio masharti ya kurejea utawala wa Sultan kama Khalifa Bin Haroub.Abdula Bin Khalifa na Jamshid Bin Khalifa Bin Haroub wa Oman?.Mimba ya tatu iliyounda jumuiya ya uamsho ni utawala wa Raisi Aboud Jumbe mwaka 1984,ambaye alifukuzwa madarakani kwa hoja ya kujadili muungano na mamlaka ya Zanzibar.Kwa vyotevyote ilibidi Aboud Jumbe asikilizwe kabla ya kufukuzwa lakini waliopeleka umbeya ule kwa mwalimu Nyerere kabla haujawasilishwa mezani,wapo uongozini haadi leo hawajasutwa kwa kuisaliti Zanzibar.Vipi uamsho wanaogopa kulisema hilo kwamba wapo waliomsaliti Aboud Jumbe na badala yake wafuasi wao waanzishe vurumai.Aboud Jumbe alitema cheche za uamsho kwa kuandika kitabu cha The partnership Tanganyika and Zanzibar Union;30 Turbulent Years, ambacho kinatumika kama muongozo wa kuvunjika kwa muungano.(rejea mdahalo wa katiba ulioitishwa na baraza la katiba zanzibar mnamo april 1,mwaka huu kwenye ukumbi wa salama hall bwawani).Khicho kimetafsiriwa katika lugha ya kiswahili na mwandishi na mwakilishi wa BBC visiwani Zanzibar Ally Saleh, ambapo kiliitwa MIAKA 30 YA DHORUBA.Naam ni mbegu hizo.Kwa mantiki hiyo ukifuatilia midahalo inayoendeshwa na baraza la katiba zanzibar,kinatumika kama turufu ya hoja za kuvunja muungano.Sijui dhamira ya Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa ni ipi?,tusisemee nafsi yake.Lakii ni mbegu iliyopandwa kwa ustadi mkubwa sana hivyo uamsho ni mtoto aliyezaliwa.Ikumbukwe Aboud Jumbe Mwimyi alikuwa raisi wa Zanzibar,mwenyekiti wa baraza la mapinduzi,makamu wa raisi na makamu wa mwenyekiti wa CCM.Hata kama Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa na kinyongo cha kutimuliwa madarakani,lakini kitabu alichotuachia kizazi chetu kinatufundisha kupanda mbegu ya nchi ya Zanzibar.Mwingine ni Dr.Harrith Ghassany ameandika kitabu cha kwaheri uhuru,kwaheri ukoloni,Zanzibar na mapinduzi ya AFRABIAswali tunalopata tangu lini Zanzibar ilikuwa na mapinduzi ya afrabia.Tangu lini jamii ya ITHNASHERI ilifurahia mapinduzi ya Zanzibar?.Hakuna jawabu ndani ya kitabu zaidi ya masimulizi tu na sijui ikiwa wasimulizi wale walimpotosha itachukua miaka mingapi mingapi kusawazisha maana nilipata kumsikia mbunge mmoja wa baraza la wawakilishi Zanzibar akisema bila kutaja kitabu hicho kwamba inahitaji kuandika vizuri mapinduzi ya Zanzibar.Bahti mbaya AFRABIA imeanza kwenye historia ya karibuni tu baada kuzaliana kwa waafrica na waarabu.Sasa mapinduzi ya AFRABIA yameanza tu hapo januari 1964 Je utawala wa Sultan wa Oman ulibarriki na kusherehekea mapinduzi ya Zanzibar hadi yaitwe AFRABIA.Hii afrabia ilijua zanzibar na ilikuwaje watu wa asili ya ustaarabu wa ETRUTIA au PHOENICIA wa Asia(tangu mwaka 800 wamehamia Africa na Ulaya)wakawa tena wakawa waasisi wa Zanzibar?.Je ujio wao pale Tunisia kirahisi tu upewe matokeo ya uwepo wao,mapinduzi ya afrabia.Yaani walijipindua,maana baba zao walikuwa waarabu mithili ya akina Tippu Tippu.Iweje kirahisi leo Zanzibar kulinganishwa na NUMIDIA(Algeria tuayoiona leo)ambayo imejaa uzao wa etrutia na phoenicia kama Sultan wa Oman?Hapana ni upotoshaji,hayakuwa mapinduzi ya AFRABIA,Uongo mtupu.Lakini hiyo nayo ni mbegu iliyozaa mtoto aitwae UAMSHO,maana inasemwa wazi kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni aina nyingine ya ukoloni,uvunjwe kila mmoja abaki na chake kisha tuungane upya,Dr.Harrith Ghassany(rejea Zanzibar Daima machi 2012)Kwa wavivu wa kutafuta historia ya kweli wataamini kila jambo lililoandikwa kwenye kitabu cha kwaheri uhuru,kwaheri ukoloni,Zanzibar na mapinduzi ya afrabia naam uzao wake UAMSHO.Waziri mkuu Mizengo Pindaalisulubiwa sana alipodai kuwa Zanzibar sio nchi,na Raisi akasazisha kwamba nje ya muungano Zanzibar sio nchi.Upesi serikali ya Mapinduzi ya Zamzibar ikafanya marekebisho ya latiba ya 10 ya mwaka 2010 na kujitangaza ni nchi kamili/taifa.Ni ibara hizo zinazotumiwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed(hana kosa anatumia vifungu vya katiba ya Zanzibar)kudai muungano uvunjwe.Baadae serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikaomba wapi bendera ya taifa na wimbo wa taifa la Zanzibar,vyote wanavyo,kwa hiyo UAMSHO imezaliwa kutokana na mbegu iliyopandwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na sehemu ya muungano,hakika haiwezi kukwepa hilo.Baraza la wawakilishi la Zanzibar likapanda mbegu ya kuzaliwa kwa UAMSHO, kwa kupitisha sheria inayomkataza mzaliwa wa Tanzania Bara kumiliki ardhi kule Zanzibar.Mnamo April 5,2012 muswada wa marekebisho ya sheria ya kamisheni ya utalii ulipitishwa kutokana na hoja binafsi ya Ismail Jussa Ladhu kuwa mzaliwa wa Tanzania bara asiajiriwe Zanzibar katika sekta hiyo.Bunge la wawakilishi likapiga kura na liliamua kwa ushindi wa kura 22 za kundi la wawakilishi wakiongozwa na Ismail Jussa Ladhu lililopendekeza kuwa watanzania bara wasiajiriwe Zanzibar dhidi ya 21 zilizopendekeza kuwa watanzania bara waajiriwe Zanzibar.Wabunge wa bunge la wawakilishi waliounga mkono kuzuia watanzania bara kunufaika na ajira Zanzibar kwa kuzingatia kifungu cha 23(3)cha muswada wa marekebisho ya sheria ya kamisheni ya utalii,Zanzibar.Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haikujua kwamba inapanda mbegu ya kuvunja muungano au haikujua kuwa inakiuka katiba ya muungano katika kifungu cha 17 (1) na ibara ya 23 (1) inayotoa nguvu kwa wananchi wote kupewa ajira kwa usawa kulingana na kazi yenyewe.Pia bunge la wawakilishi hakujua kwamba linapingana na Azimio la jumuiya ya Africa Mashariki,ambapo Tanzania imeridhia?Wazanzibar wanachofanya ni national actor kama wafanyavyo jamhuri ya kiislamu ya Iran,wanatafuta uhai wa maisha yao ndio maana wanaona lazima wawafukuze watanzania bara na baadae wavunje muungano,Ikumbukuwe mwakilishi wa mji mkongwe Ismail Jassu Ladhu aliongoza hoja za kupinga serikali ya muungano iliyohitaji nyongeza ya eneo la Tengefu la kiuchumi,baada ya timu ya wataalamu iliyoongozwa na Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi Prof.Anna Tibaijuka,kwenda umoja wa mataifa(uno)kupata kibali.Mh.Jussa Ladhu alipingana na serikali ya muungano na alidai suala hilo liliamuliwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia baraza la wawakilishi.Washirika wengine wamejitokeza kwenye kitabu cha KATIBA TUITAKAYO ni ZIORI(Zanzibar Indian Ocean Research Institute)ZLC (Zanzibar Lawy Society)ZAFE (Zanzibar Female Laywers association) ZLSC (Zanzibar Legal Service Centre)na WAHAMAZA (Waandishi wa habari za maendeleo ya zanzibar)Naaam....kwa hiyo serikali ya mapinduzi ya zanzibar ikapinda mbegu,watu binafsi wamepanda mbegu na asasi mbalimbali zikapana mbegu na mtoto amezaliwa anaitwa UAMSHO.Msilie wala kulaumu,bali ni mrejesho tu.
ZANZIBAR NA MWELEKEO WA SCOTLAND.
Wakati mwingine baadhi ya vipande vya nchi vinadhani kuwa ili viweze kujitegemea lazima,vijitenge kutoka nchi waliyomo.Sudan Kusini ikiamua kupiga kura ya kujiondoa kutoka Sudan moja,hivyo kuunda mataifa mawili,Sudan ya kusini na Sudan ya kaskazini.Matokeo yake mataifa haya yametangaziana ubaya na uhasama wa umwagaji damu.Bunge la Sudan ya kaskazini limepitisha azimio la la uhasama dhidi ya Sudan kusini kisa ni utajiri wa mafuta.Sio mipango ya Mungu(an act of god)bali ni binadmu.Harakati za Zanzibar kuanza kuchokonoa Muungano zinahusishwa na kauli zilizowahi kutamkwa na hayati Karume kwamba muungano ni kama koti linalobana unaweza kulivua.Nimeyaona na kusika hayo kwenye mdahalo wa katiba ya Zanzibar,hivyo kama sio busara za Ally Saleh,mwandishi wa BBC na mwenyekiti wa baraza hilo Prof.Abdul Sherrif basi mdahalo ule ungekuwa uwanja wa vita.Wengine walikwenda na kutamka kwamba hata viongozi wa Zanzibar watakabiliwa na maasi ikiwa watazuia vuguvugu la kuundwa kwa jamhuri ya watu wa Zanzibar.Je walimaanisha wapo tayari kuingia msituni kuidai Zanzibar yao.Kwa harakati zinazoendelea Zanzibar zinalingana na za Scotland katika United Kingdom.Waziri mkuu wa Scotland ALEX SALMOND wa chama cha SNP(scotland national party)yupo mstari wa mbele kuvunja muungano wao.Scotland inataka kujiondoa kutoka United Kingdom, na kuziacha Wales,England na Ireland Kaskazini.Kamoeni zinaendelea lakini inadaiwa kuwa 57% ya wananchi wanapinga ajenda hiyo ya kujitoa katika muungano huo ifikapo mwaka 2014 wakati wa upigwaji kura za maoni,kuamua Scotland iendelee na muungano au ijitoe.Miongoni mwa ajenda za kujitoa kwenye muungano ni gesi na mafuta yanayopatikana chini ya bahari ya Kaskazini katika mpaka wa Scotland na England,kama ilivyo kwa Zanzibar.Ni nyayo zilezile za uchoyo zinawafanya waamini kuwa tatizo la hali duni linasababishwa na muungano.Bahati mbaya hawapo tayari kujadili hoja kwa staili hiii ya leo,bali wanashikilia kauli za marehemu nyenzo ya kuvunja muungano.
ZANZIBAR KAMA ERITREA?
Zamani Puntland na Somaliland zilikuwa ndani ya Somalia yaani nchi moja.Lakini zote zimebaki kwenye migogoro isiyo na kichwa wala miguu,maana sasa ni nchi tatu tofauti.Hii inatukumbusha kisa cha Ethiopia na Eritrea zilikuwa na muungano kabla ya kusambaratika baaadae.Ethiopia na Eritrea zilikuwa na muungano ambao unafanana na Tanganyika na Zanzibar.Eritrea ilitawaliwa na Italia hadi mwaka 1941 waliposhindwa vita na Uingereza.Baadaye Uingereza ikaruhusu Eritrea kujitawala kama nchi huru chini ya usimamizi wake.Hapo ndipo vikaanzishwa vyama vya wafanyakazi na vyombo vya habari huru.Mwaka1952 wakafanya majadiliano juu ya hatima ya Eritrea.Ethiopia ilidai ipewe nchi hiyo (Eritrea)sababu kihistoria ilikuwa sehemu ya ufalme wa Ethiopia.Lakini ukazuka ugomvi,nchi jirani za kiarabu zilitaka Eritrea iwe nchi huru.Kipindi hicho Eritrea ilikuwa na watu 3,000,000 tu,lakini waliogawanyika.Wakristo na kabila la Tigraya waishio karibu na mji mkuu Asmara,waliunga mkono muungano na Ethiopia.Nusu iliyobaki wallikuwa Waislamu waishio ukanda wa jangwani karibu na bahari ya Sham na bonde la magharibi walitaka uhuru (kuunda Eritrea).Umoja wa Mataifa ukasimamia kuunda muungano wa shirikisho la Ethiopia na Eritrea.Hivyo wakakubaliana kuwa serikali ya Ethiopia isimamie mambo ya nje,ulinzi,fedha,biashara,bandari na forodha.Muundo wa muungano ule upo sawa na wa Tanganyika na Zanzibar.Eritrea kama Zanzibar iliruhusiwa kuwa na bendera yake,lugha za kitaifa,kitgraya na kiarabu.Mtawala wa Ethiopia HAILLE SELASIE kwa muono wake ulikuwa kama wa Mwalimu J.K.Nyerere wa Tanzania,kwamba muungano ule ni hatua za mwanzo za kuunda nchi moja.Kero na kelele juuu ya muungano zilianza kusikika kwa watawala wa Ethiopia.Ubaguzi ukachukua mkondo,wanasiasa wa kitigraya walipoanza kuvuka mipaka ya mambo yaliyokubaliwa chini ya mkataba wa muungano kwa kuongeza mambo kwa njia ya shinikizo,vitisho na uthibiti wa Waeritrea.Nao Waeritrea wakaona muungano ni kero ndipo kelele dhidi ya Ethiopia kutaka kuimeza Eritrea kama Wazanzibar wanavyolalamika kumezwa na Tnaganyika.Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifikia mambo 11 tu,baadhi yakiwa kama yaleyale yaliyokuwa kwenye muungano wa Ethiopia na Eritrea.Hivyo Eritrea ilisimamia mambo yote yasiyo ya muungano.Baadaye Eritrea ilitoa madai ya msingi
(i)kufutwa kwa bebdera yao mwaka 1958 na watawala wa Ethiopia.
(ii)kufutwa kwa vyama vya wafanyakazi na vyama vya siasa mwaka1959
(iii)mwaka 1962 bunge la Eritrea lilishikinikiza kukubali kufutwa kwa shirikisho na bunge la na kulazimishwa kujifuta lenyewe ili Eritrea imezwe na Ethiopia,hivyo ikahesabiwa kuwa jimbo la Ethiopia.
Lakini kwa Zanzibar hakuna jambo kama hilo kwani ina bendera,wimbo wa taifa na kadhalika.Eritrea ikaamua kuingia msituni,licha ya kuchapwa mara kadhaa waliendelea na vita hadi mei 1991 mtawala wa Ethiopia mfalme Mengstu Haille Mariam alipotoroka nchi yake baada ya kupigwa na majeshi ya muungano wa Eritrea na Tigraya.Kura ya maoni ya julai 1991 chini ya umoja wa mataifa ikatangazwa kuwa Eritrea ni nchi huru. na mwaka 1993 ikatambuliwa rasmi baada ya kuhangaika kwa miaka 30.Zanzibar haijanyangwa chochote,lakini kelele ni nyingi mno,walalamikaji ni wengi.Hofu yangu,siku Tanganyika ikipaza sauti yake,ukimya wao sio bure kuna jambo polepole litaibuka.TAFAKARI;Kama watu wa Zanzibar wanaona hivyo......,mimi siwezi hata kidogo kuwaua wananchi wa Zanzibar.Kama waliingia katika muungano kwa hiari yao,wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao.Hatukuishinga Zanzibar vitani (uk.154,rejea nyerere of Tanzania:The first decade 1961-1971,kimendikwa na Wiliam Smith)
No comments:
Post a Comment