MAPINDUZI YA AFRIKA - LEKULE

Breaking

14 Apr 2014

MAPINDUZI YA AFRIKA




MAPINDUZI YA AFRICA


AFRICAN REVOLUTIONS

Kwa kipindi cha miaka mitano sasa hali ya kisiasa ya barani Africa imeendelea kuwa tete.Mabadiliko makubwa ya kisiasa kwa baadhi ya nchi za kiafrica yamesababisha viongozi wakongowe na majabali kuangushwa kwenye sanduku la kura,maandamano ambayo yamewalazimsha kujiuzulu nyadhifa zao au kutokana na afya mbaya zilizowakuta,pamoja na kupinduliwa kwa baadhi ya serikali.Suala la mapinduzi linaonekana kuchukua nafasi kubwa katika siasa za Africa nyakati hizi.Kana kwamba historia inajirudia kwani ktk miaka ya 1960 kuliwepo kwa mapinduzi ya serikali mbalimbali AFRICA.Mathalani Nigeria ni nchi ambayo kwa miaka mingi iliongozwa na wanajeshi ambao walifanya mapinduzi dhidi ya wenzao.NANDI AZIKIWE,LUTENI KANALI OLUSEGUN OBASANJO,JENERAL OWOLOWO,SANI ABACHA,JENERAL SHENGARI,MEJA JENERAL MAHAMUDU BUHARI,MEJA JENERAL IBRAHIM BABANGIDA,JENERAL GOWON,BRIGEDIA MURTALA RAMAT MUHAMMED & LUTENI KANALI ODEMEGWU OJUKWU[alitangaza uhuru wa biafra]

Nchini Comoro,baada ya uhuru iliongozwa na raisi ALI SOILIH,Naye alipinduliwa na AHMED ABDULLAH,ambaye aliungwa mkono na UFARANSA.Hata hivyo AHMED ABDULLAH aliuawa mwaka 1989 nchini AFRICA KUSINI.Baada ya kifo chake ndipo SAID MOHAMED DJOHAR aliteuliwa kuwa raisi wa comoro lakini nae alipinduliwa na BOB DENARD[mfaransa liyetumika kupindua serikali mbalimbali kupitia idara ya FRANCAFRIQUE]Mwaka 1996 MOHAMED TAKI ABDULKARIM alichaguliwa kuwa raissi wa comoro.Uchaguzi wake ulikuwa wa kidemokrasia kwani kwa mara ya kwanza nchi hiyo ilifanya uchaguzi badala ya kupinduana.Yeye alifanikisha uuundwaji wa katiba mpya na mambo mengi yenye kukumbukwa na wananchi wa comoro.Hivyo basi kabla ya demokrasia kuchukua mkondo wake.Comoro ilipitiwa na wimbi la mapinduzi ya kijeshi.

Nchini NIGER kulitokeamapinduzi salama kwanjia ya sanduku la kura.Raisi MUHAMANE OUSMANE wa chama cha AFC[aliances des fotces du changement] alipigiwa kura ya kutokuwa na imani nae[VOTE OF CONFIDENCE] na bunge la nchi hiyo.Kutokana na kura hiyo ya mwaka 1994,mapema january mwaka 1995 OUSMANE aliacha nyadhifa yake.KWAME NKRUMAH alikumbana na mapinduzi ya kijeshi february mwaka 1966 na kundi lililojiita BARAZA LA UKOMBOZI LA TAIFA.Baadae KOFI A BUSIA aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa GHANA.Yeye alikuwa kiongozi wa chama cha upinzni cha UP,kama inavyosemwa aliyeingia kwa upanga atatolewa kwa upanga.Mwaka 1971 GHANA ilikabiliwa na kuporomoka thamani ya fedha yao hivyo kuzorotesha masuala ya uchumi wao.Hali hiyo ilimweka pabaya sana KOFI A BUSIA na kulega kw serkali.Mwaka 1972 yalifanyika mapinduzi mengine dhidi yake ambapo KANALI IGNATUSI K ACHEAMPONG,alifanikisha kumuondoa madarakani.Mwaka 1978 mapinduzi mengine yalijitokeza,ambapo IGNATIUS alipinduliwa na nafasi yake kuchukuliwa na JENERAL FREDRICK W AKUFFO.nae alipinduliwa na JERRY JOHN RAWLINGS.Yeye aliachia madaraka baadae ili uwepo utawala wa kiraia.Ndipo mwaka 1979 wananchi wa ghana wakamchagua HILLA LIMMAN kuwa rais mpya.Kama ilivyo kwa wengine waliotangulia kupinduliwa,HILLA LIMMAN hakudumu akapinduliwa mwaka 1981 na JERRY JOHN RAWLINGS.Miaka michache baadae JERRY aliitisha uchaguzi ambao alishinda na kuwa mtawala wa kiraia.MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE aliwahi kukutana na wimbi la nia ya kumpindua.Mwaka 1964 na 1984 baadhi ya wanajeshi walipanga njama za mapinduzi lakini hazikufanikiwa.Kimsingi nchi nyingi zilikabidhiwa na wakati mgumu kutokana na mapinduzi yaliyojitokeza.MAPINDUZI hayo yanaonekana kujirudia kwa baadhi ya nchi hapa AFRICA.Kwa kipindi hiki sababu zinaelezwa ni kutoridhushwa na mwenendo wa serikali zilizopo madarakani kwani zinakabiliwa na RUSHWA,WIZI,UONGOZI MBOVU,KUSHINDWA NA KUZOROTESHWA MAENDELEO.Kuna mifano ya karibuni iliyojitokeza hapa AFRICA.

1.MARC RAVALOMANANA[MADAGASCAR]
Mtindo alioingia nao madarakani wa mapinduzi ndio uleule ulimuondoa madarakani.Bahati mbaya kwake mapema mwaka huu ndege aliyopanda kutoka AFRICA KUSINI ilikataliwa kutua uwanja wa ndege wa ANTANANARIVO kutokana na amri ya RAISI RAJAJOELI.Ravalomanana aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi na jeshi mwaka2009 huku wananchi wakiendesha maandamano ya kuunga mkono harakati hizo.Baadae ANDRY NIRINA RAJOELINA aliteuliwa kuwa raisi wa nchi hiyo,ambae zamani alikuwa mchezesha muziki[dj].Rajoelina aliwahi kuwa meya wa jiji la Antananarivo.Mahali hapo ndipo palimuweka ktk nafasi nzuri ya kuteuliwa kuwa raisi baada ya kuondolewa kwa RAVALOMANANA.Tukirudi nyuma tunaona PHILBERT TSIRANANA alipinduliwa kwa nguvu za umma hivyo akajiuzulu ma mafasi yake ikachukuliwa na JENERAL GABRIEL RAMANANTSOA mwaka 1972 Naye hakudumu kwani mwaka 1975 alipinduliwa na LUTENI DIDIER RATSIRAKA.Safari hii mapinduzi ya nguvu ya umma yalimuondoa madarakani LUTENI DIDIER RATSIRAKA na nafasi yake ikachukuliwa na ALBERT FAZY mwaka 1993.Lakini mapinduzi ya nguvu za umma yaliyoanza kwa kuipinga serikali ya LUTENI DIDIER yalifanywa na sanduku la kura na kumpatia ushindi ALBERT ZAFY.Hata hivyo LUTENI DIDIER alirejea madarakani mwaka 1997 baada ya kumshinda ALBERT ZAFY.Naam ilikuwa ni kupinduana kijeshi na kwa njia ya ngguvu za umma.Ni nguvu inaweza kutokea nchi yoyote duniani.


2.ZINE EL ABIDINE BEN ALI[TUNISIA]
Raisi huyu aliangushwa madarakani baada ya maandanamano makubwa yaliyoitishwa nchi yake,baaada ya kijana MOHAMED BOUAZIZI kujichoma moto ktk mji wa SIDI BOUZID [26] huko tunisia.Sababu za kujichoma moto zinaelezwa ni kutokana na kunyanyaswa na askari wa mji huo ambako alikuwa akifanya biashara yake ya matunda.Ikumbukwe kuwa kijana huyo alikuwa ni miongoni mwa wahitimu wa chuo kiukuu wasio na ajira.Rais BEN ALI alipinduliwa kwa nguvu za umma na wananchi wa TUNISIA waliochukua hatua kali dhidi ya serikali yake.Licha ya wananchi kupigwa mabomu na risasi na jeshi la polisi,hivyo kuwaua watu 50 bado haikumuokoa raisi huyo kuondoka madarakani.Mwishowe jeshi la polisi la tunisia lilishindwa kupambana na wananchi,likasalimu amri na kuweka silaha chini na kuachia maandamano ya amani kupinga sreikali ya raisiBEN ALI,Baadae raisi BEN ALI aling`atuka madarakani na kukimbilia uhamishoni,lakini alijikuta akihaha angani[ndani ya ndege]kuomba walau atue chini nchini UFARANSA lakini alikataliwa.Raisi BEN ALI alichukua madaraka kutoka mikono mwa baba wa taifa wa tunisia HABIB BOURGUIBA.BEN ALI awali alikuwa kiongozi wa chama cha RDC[rassenblement construtuionel democratique] na alitwaa madaraka mnamo novemba 7 1987,baada ya taarifa za kitabibu kusema HABIBU hataweza kuiongoza nchi hiyo tena.Tangu january 8 hadi 10 2011 maandamano yakatamalaki nchini tunisia.Hatimae january 14 2011 raisi BEN ALI akaikimbia nchi.Mapinduzi yaliyomng`oa yanaitwa JASMINE REVOLUTION.


3.HOSNI MUBARAKI[MISRI]
Maandamano makubwa ya wananchi yaliyofanywa dhidi yake yalisababisha akubali kujiuzulu madaraka yake.Wananchi walikesha ktk viwanja vya TAHHIR[TAHHIR SQUARE]wakishinikiza kutatuliwa kwa hali ngumu ya maisha ambayo raisi MUBARAK alishindwa kufanyia kazi masuala hayo.Mkuu wa kijeshi MOHAMED TANTAWI aliamuru jeshi la nchi hiyo kutokufyatua risasi zozote dhidi ya wananchi.Pia aliwaomba wananchi waandamane kwa amani kushinikiza madai yao dhidi ya raisa MUBARAKI.Baadae raisi huyo alijiuzulu huku MOHAMED TANTAWI akiongoza nchi kwa muda.Hatua hiyo ilichangia kufanyika kwa uchaguzi wa huru na wa haki ambao umekifanya chama cha MUSLIM BROTHERHOOD kuongoza viti vingi vya bunge la misri.Nguvu ya umma iliyomng`oa MUBARAK ni kama ilivyomng`oa NICOLE CEAUSESCU wa Romania,ambapo mji wa BUCHAREST ulitawaliwa na maandamano makubwa hadi alipojiuzulu.



4.LAURENT GBAGBO[IVORY COAST]
Alikuwa raisi wa ivory coast yeye aliangushwa na ALLASANE QUATARA,lakini alikataa kutambua ushindi wa mpinzani wake.Aidha aliendelea kung`ang`ania madaraka hatua ambayo ilizua mzozo kwa wananchi.Mzozo huo ulimalizika aprili 11 2011 pale vikosi viitiifu kwa QUATARA vkisaidiwa na wanajeshi kutoka nje ya nchi vlipovamia handaki lake na kumkamata.Mapigano baina ya GBAGBO NA QUATARA yalisababisha mamia ya wananchi wa ivory coast kuikimbia chi yao.Mapigano makali yalizuka ktk mji wa abdijan na duekoune.Mji wa deukone ulikuwa ngome ya wafuasi wa gbagbo.Hata hivyo gbagbo anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita ktk mahakama ya kimataifa [ICC]kosa lake kubwa lilikuwa kung`ang`ania madaraka.Jambo la aibu ni kutokana na vikosi vya jeshi vilivyovitiifu kwa QUATARA vilifanikiwa kumtia mbaroni gbagbo aliyejificha kwenye handaki akiwa na fulana pekee.Lakini tukio chafu na alikamatwa na mkewe.Wachambuzi wa siasa wanasema alifanya uzembe wa hali ya juu licha ya kuwasikiliza washauri wake au mkewe.Kwa sasa anayo kesi ya kujibu tangu aangushwe.

5.RUPIAH BANDA [ZAMBIA]
MICHAEL SATA ni mwanasiasa ambae kwa muda mrefu alishiriki ktk kikyang`anyiro cha uchaguzi wa raisi wa nchi hiyo bila mafanikio.Alishindana na LEVY MWANAWASA lakini hakufanikiwa,Hata hivyo MICHAEL SATA alifanikiwa kumuangusha RUPIA BANDA ktk uchaguzi uliofanyika mwaka jana.Kuangaka kwa RUPIA BANDA kisha kukubalia matokeo kulileta picha bora kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara n ajumuiya ya SADC kwa ujumla.RUPIAH BANDA alikubali kushindwa mbele ya MICHAEL SATA ambae sasa nndie raisi wa ZAMBIA.




6.CANAL GADDAFI[LIBYA]
Waasi wa mji wa BENGHAZI walitukumbusha historia ya mwaka 1969,Canal GADDAFIalimpindua mfalme IDRISS wa benghaziambae alikuwa mfalme wa libya.Wakati Gaddafi akifanya mapinduzi hayo alikuwa akitokea chuoni LONDON.Wakati huo libya alikuwa na muungano wa TRIPOLITANIA NA CYRENAICA.Maeneo hayo mawili tangu zama za ukoloni yaligawanyika Cyrenaica ilikuwa chini ya utawala wa kigiriki,halafu Tripolitania ilikuwa chini ya utawala wa Warumi.Kwa Tripolitania ilianzishwa na familia ya Quaramanli halafu Cyrenaica alianzishwa na Wahhabi.Ktk historia ni kwamba waarabu na watu wa makabila ya Berber ndio walitengeneza sura za watu wa africa ya kaskazini ambapo mwaka 1940 walikuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza.Sasa kupinduliwa kwa Gaddafi mwaka 2011ni kama historia kujirudia.Waasi wa benghaz walipata nguvu kubwa kutoka kwa majeshi ya NATO.Harakati zao zilianzia ktk mji wa benghaz hadi Sirte alipozaliwa Gaddafi.Mapambano ya miezi kadhaa yalimuangusha Gaddafi na kumuua.Gaddafi alikuwa mwamba wa kaskazini ambao ulikuwa na mipango mingi ya maendeleo kwa bara la Africa.Lakini makosa yake ktk utawala yalimgharimu na kuchukua uhai wake.Mwanae SAIF AL ISLAM huku mahakama ya kimataifa ya uhalifu ikisema haitampeleka THE HAGUE UHOLANZI kusikiliza kesi yake imeachwa iendelee libya.Kwa sasa hali ya libya ni mbaya.Mapigano baina ya makundi ya wapiganaji wa kabila la TOUBOU yanaendelea mjini SAbha na yamekuwa makubwa kiasi ambacho wanatumia ROCKET.

No comments: