Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema Mh.Zitto Kabwe leo ametinga mahakama kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es salaam kuweka pingamizi la la kisheria kuzuia Mkutano wa kamati kuu ya CHADEMA uliopangwa kufanyika tarehe 3/1/2014.
Zitto kupitia kwa Wakili wake Albert Gabriel Msando aliwasilisha aliwasilisha pingamizi hilo kwa hati ya dharura iliyosainiwa na wakili Msando.Pingamizi hilo limesikilizwa leo na Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Jaji Uttamwa.CHADEMA iliwakilishwa na jopo la mawakili lilioongozwa na wakili Tundu Lissu,ambae ni mwanasheria Mkuuu wa CHADEMA.
Hoja ya Mh.Zitto zililenga kuzuia mkutano mkuu wa kamati kuu ya CHADEMA uliopangwa kusikilizwa kesho ukiwa na ajenda kuu tatu ikiwamo ya kupokea utetezi wa mdomo wa wanachama watatu wa CHADEMA wanaotuhumiwa kukiuka kanuni na taratibu za chama,Zitto,Samson Mwigamba na Dr.Kitira Mkumbo.
Hoja za Zitto ni kuwa kikao cha kamati kuu ya CHADEMA cha kesho kitazuia kusikilizwa kwa rufani yake aliyoiwasilisha Baraza kuu akipinga kuvuliwa kwake nyadhifa ndani ya chama bila ya kusikilizwa.Hii ni kusema Zitto alishaadhibiwa bila ya kujibu tuhuma dhidi yake.
Wakili Msando,kiujumla amejenga hoja kuwa kikao cha CC ya CHADEMA cha kesho kisijadili jambo lililokwisha kukatiwa rufaa na hivyo rufaa isikilizwe kwanza na baraza kuu.Ya kwamba tuhuma 11 ni tuhuma mpya na trayari Zitto ameshaadhibiwa pasipo kutenda jambo lolote na kusikilizwa popote.
No comments:
Post a Comment