KWAHERI 2013,KARIBU 2014 KIROHO SAFI KABISA. - LEKULE

Breaking

31 Dec 2013

KWAHERI 2013,KARIBU 2014 KIROHO SAFI KABISA.

Mwaka 2013 ulianza kwa wema kabisa kwangu pamoja na jamaa,ndugu na marafiki zangu wote kwa pamoja tulianza safari yetu ya maisha ya mwaka 2013 kwa wema kabisa,matatizo ni sehemu ya maisha na ili maisha yakamilike kuitwa Maisha lazima yaambatane na MATATIZO,kwa uwezo wake mungu yaliweza kutatuliwa kwa kadri uchumi wetu ulivyoruhusa ingawa mengine bado yapo yanaendelea na imani yangu kuwa mengine mengi yataendelea kujitokeza nayo yatatuliwa kwa kadri itakavyowezekana.

TATHIMINI YANGU INGAWA KWA UCHACHE
Tathimini yangu hii imegawanyika katika vipengele vichache ambavyo vinanihusu kwa namna moja ama nyingine katika safari yangu ya 2013,

MARAFIKI,NDGU NA JAMII
Nashukuru kwamba mwaka huu niliutumia kutengeneza marafiki wenye nia njema na kuwafuta wenye nia na mawazo mabaya,nilitengeneza marafiki nilionana nao macho kwa macho,kupitia mitandao ya kijamii kama facebook,twiter,whats`App,youtube,email na n.k,wapo niliokutana nao katika safari zangu za hapa za ndani na nje ya nchi,niliokutana nao katika shughuli za kijamii katika kulijenga taifa letu tukufu,na wengine wengi nawatakia kila la kheri katika maisha yenu na muendelee kuonyesha ushirikiano mwema bila kuwasahau marafiki zangu wa Ivory Coast na Namibia.

NILIYOJIFUNZA.
Nimejifunza mengi sana ila kikubwa nilichofunzwa na kukifurahia ni jinsi ya utengenezaji na utendaji kazi wa biogas na nimejifunza vya kutosha na naelewa sana jinsi ya kufanya utengenezaji na utendaji kazi wake vizuri sana.Hili nilifunzwa na CARMATEC kwa ufaddhili mkubwa wa REA.Shukrani nyingi kwa Mwalimu wangu ENGINEER,DOCTOR INOCENT MJEMA wa CARMATEC-ARUSHA,wengine ni SEMI SENGOKA NA MUSTAPHA hawa walikuwa waalimu wangu wa PRATICALS,Shukrani nyingine ni kwa DADA AGNES wa REA makao makuu DAR-ES-SALAAM.

YALIYONIHUSUNISHA KITAIFA
Jmano lililonihusunisha zaidi kitaifa ni lile la OPERSHENI TOKOMEZA MAJANGILI,binafsi nilibahatika kutazama video na picha za zale yaliyotokea katika operesheni ile na yalinisikitisha kiasi kwamba sitamani tena kuiona au kuisikia katika akilia yangu.Pia ajali ya basi la abiria la kampuni ya BURUDANI nayo ilinihusunisha sana katika nafsi yangu naumia sana.

YALIYONIFURAHISHA KITAIFA.
Ni tukio la Raisi wa Marekani kukanyaga katika ardhi ya Tanzania nategemea fursa nyingi kutokana na safari yake,pia taifa langu kutimiza miaka 52 ya uhuru wake ingawa uchumi wake ni wa kujikongoja.Harakati za kisiasa zinazoendeshwa na vyama vya upinzani ambazo zinawafanya viongozi wa kiserikali kuwajibika kupita maelezo na kufanya uchumi na maendeleo ya taifa ili kutembea mbele ingawa ni kwa spidi ya kinyonga lakini inatosha kwanipole pole ndio mwendo.


KIBURUDANI KWA NDANI YA TAIFA TANZANIA
1.SOKA/FOOTBALL
Nilifurahi sana siku amabayo timu ya taifa TAIFA STARS ilipoifunga timu ya Morocco 3-1,jingine ni siku amabyo timu yangu ya SIMBA ilipoilazimisha watani wetu YANGA kwa ushindi wa 3-3,pia ni pale SIMBA ilipoifunga YANGA 3-1 katika mechi ya bonanza ya NANI MTANI JEMBE.

2.MUZIKI/MUSIC
Nimekuwa mpenzi na mshabiki mkubwa wa HIP HOP ya kibongo na hakuna msanii anarap nisimpende na msanii nilitokea kumkubali zaidi kwa mwaka huu ni YOUNG KILLER(MSODOKI)Wengine ni YOUNG DEE,DOGO JANJA,STAMINA,ROMA,IZO B,NYANDU TOZII,NAY WA MITEGO,WEUSII,
Style ya Azonto nayo imekuwa ikinivutia sana napoingia club.
Deejayz ni Dj Choka,Dj Haazu,Dj Mwanga,Dj Zirro
Radio Presentere ni Moko Biashara,Gadna G Habbash Yussuph Magasha,Baba Jonii
Bongoflavour ni Linex,Recho,Amini,Barnaba


KWAHERI 2013



KARIBU 2014.












No comments: