Tanzania Yachafuliwa Burundi.......Yatuhumiwa Kupitisha Silaha Bandarini Dar es Salaam


RAIS Dk. John Magufuli ameombwa kuzuia upitishwaji wa silaha za kivita zinazodaiwa kupitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchini Burundi.

Ombi hilo lilitolewa mjini hapa jana na vyama sita vya wanaharakati wa haki za binadamu na kiraia vilivyowasilisha maombi yao mbele ya Kamati ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) inayoendelea kusikiliza maombi hayo mjini hapa.

Wanaharakati hao wameiambia Kamati hiyo ya Bunge kwamba, silaha hizo zinazodaiwa kupitia nchini Tanzania hutumiwa na Serikali ya Burundi yakiwamo makundi ya vijana wanaodaiwa kuiunga mkono Serikali.

Mbele ya Kamati ya Migogoro na Usuluhishi ya Bunge la Afrika Mashariki, Rais wa Muungano wa raia wa Burundi wanaopinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza, Vilalis Nshihirimana, alidai silaha hizo zimechangia umwagaji wa damu nchini humo.

Alisema zipo taarifa za uhakika kuwa silaha hizo zimekuwa zikipitia Dar es Salaam ambako kwa nchini Burundi hali ya usalama imeendelea kuzorota huku mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na vyombo vya Serikali ikiwamo polisi, jeshi na makundi ya vijana yakiendelea kushamiri.

“Tunamuomba Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania wazuie silaha hizo kuingia Burundi kupita Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Nshihirimana na kuongeza:

“Taarifa hizi za silaha kuingia Burundi kupitia Dar es Salaam ni za uhakika na tumezipata kutoka kwa watoa taarifa wetu ambao tunalazimika kuwalinda lakini ni kweli silaha zinaweza kuingizwa kwa kupitia hata ndege zinazoenda Burundi lakini ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuna usalama wa kutosha kwa wananchi wa Burundi,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa EALA, Dora Byamukama kutoka nchini Uganda, aliomba kupewa ushahidi wa tuhuma hizo.
 
Naye mbunge wa EALA kutoka nchini Burundi, Hafsa Mossy, aliwataka walalamikaji hao kueleza silaha hizo ziliingizwa na akina nani na kuwataka kuzungumzia silaha zilizozagaa na zinazotumiwa kushambulia miundombinu na maofisa wa Serikali zinatoka wapi.

Kwa upande wake Mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Adam Kimbisa, aliwataka wanaharakati hao kuacha kutoa kauli zisizo na ushahidi na zinazoweza kuvuruga uhusiano baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Haya madai ni very sensitive (nyeti mno) na isitoshe hayana ushahidi wowote kwa kuwa hakuna arms embargo (vikwazo vya silaha) ilivyowekewa Burundi na pia silaha zinaweza kuingizwa hata kwa kutumia usafiri wa ndege, sasa tusianze kunyoosheana vidole wakati tunatafuta suluhu ya mgogoro wa jirani zetu,” alisema Kimbisa.

Wanaharakati hao wanawasilisha maombi kwa Kamati hiyo ya Bunge la EALA ya kutaka Bunge hilo likutane kujadili na kuutolea azimio mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi tangu Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza azma ya kuongeza muhula wa tatu wa kuiongoza nchi hiyo.

Wakati wanaharakati hao wakitoa madai hayo dhidi ya Tanzania, mwishoni mwa mwaka jana Serikali ya Burundi ilidai kukamata silaha nyingi kutoka kwa wafuasi wa upinzani.

Ilidaiwa kuwa waliokamatwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha FNL kinachoongozwa na Agathon Rwasa.
 
Kukamatwa kwa silaha hizo kulitokana na kundi la watu wenye silaha kudaiwa kuingia nchini humo.

Ilidaiwa wakati watu hao wakikabiliana na jeshi la nchi hiyo katika Mkoa wa Kayanza, Kaskazini mwa Burundi, polisi walifanikiwa kukamata bunduki thelathini katika kijiji kimoja cha Mkoa wa Muyinga, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Siku chache baadaye polisi hao hao walidai kukamata silaha nyingine kutoka kwa vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD.
 
Kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara nchini Burundi kati ya kundi la watu wenye silaha na vikosi vya usalama na jeshi la nchi hiyo.
 

Pamoja na kwamba vyombo vya usalama vimekuwa vikidai kudhibiti hali hiyo, hata hivyo uchaguzi uliomuingiza madarakani Rais Nkurunziza hivi karibuni umeamsha hasira kubwa hususani kutoka kwa wapinzani wake na hivyo kuzua hali ya shaka.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF