Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Ziara Ya Katibu Mkuu (mawasiliano) Ya Kutembelea Shirika La Posta Tanzania


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora alifanya ziara ya kutembelea Shirika la Posta Tanzania ili kufahamu utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu ya Shirika. 
Katika ziara hiyo Prof. Kamuzora aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wake Dkt. Maria Sasabo na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Shirika hilo. 
Katika ziara hiyo Prof. Kamuzora alimuagiza Kaimu Posta Masta Kuu wa Shirika la Posta Tanzania Ndugu   Fortunatus Kapinga kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa mapato yote ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) nchi nzima yanafanyika kwa kutumia njia ya elektroniki ambapo alisema kuwa, “Shirika liboreshe mifumo yake ya kielektroniki ili kupunguza mianya ya wizi na upotevu wa fedha za Shirika na kufanikisha ongezeko la ukusanyaji wa mapato ya Serikali”. 
Prof. Kamuzora aliongeza kuwa Shirika la Posta Tanzania liendane na mabadiliko ili liende kuwahudumia wananchi wa sasa na wa vizazi vijavyo. Shirika ni la kipekee na lina nafasi nzuri ya kutoa huduma kwa wananchi kama ambavyo Shirika kama hili linafanya kazi nzuri  kwenye nchi ya China na Brazil.

Aidha, Prof. Kamuzora aliwaagiza Viongozi wa wasimamizi wa Shirika la Posta Tanzania kutumia Sheria, Kanuni na taratibu za kuwasimamia wafanyakazi na kuwachukulia hatua kali na za kinidhamu watumishi wazembe; wasiotimiza majukumu yao; wasio waaminifu na wabadhirifu.
 Aliongeza kuwa watendaji wafanye kazi na kusimamia Shirika kwa kuwekeana malengo kama inavyojulikana kisheria kwa kutumia Mfumo wa wa Wazi wa Upimaji Utendaji Kazi (OPRAS). 
Alisisitiza kuwa, “Sheria zilizopo zinatosha kumsimamisha mtumishi kazi kwa makosa na hatimaye kumfukuza kazi kwa kuwa watumishi wazembe na wasio waadilifu wanawafanya wananchi wawe na mtazamo hasi na Serikali yao”. 
Prof. Kamuzora alisema kuwa wateja wanahitaji huduma nzuri; ya uhakika na kufikishiwa vifurushi, barua, vipeto na bidhaa nyingine kwa wakati. 
Aliwaagiza viongozi wa Shirika kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za uendeshaji ili kuendesha Shirika kwa tija na faida. Prof. Kamuzora alisema, “Uchumi wa nchi hauwezi kukua wala kwenda popote bila kufanya kazi kwa tija."
Alivitaka vyama vya wafanyakazi visiwatetee watumishi wazembe na vishirikiane na Serikali kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika na watumie mtandao mpana wa Shirika uliopo nchi nzima na kuangalia fursa zilizopo ili kufikisha huduma kwa wateja.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Mawasiliano ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wake Dkt. Maria Sasabo aliagiza kuwa, “Shirika lijipange haraka na kuongeza kasi ya utendaji kazi ya kuwahudumia wateja wake na wananchi ili kuweza kuendana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli”. 
Dkt. Maria Sasabo aliongeza kuwa Shirika la Posta lipo nchi nyingi duniani na bado linahitajika hivyo ni muhimu kujipanga kuendana na mahitaji ya sasa ya wateja na Shirika libadilishe utaratibu wa utendaji kazi na kuondoa urasimu ili kuweza kuwahudumia wateja. 
Dkt. Maria Sasabo aliwaagiza viongozi wa Shirika wafanye tathmini na kuangalia namna bora ya kujiendesha ikiwemo kupitia upya muundo na majukumu ya Shirika.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Mawasiliano Prof. Kamuzora aliuagiza uongozi wa Shirika la Posta Tanzania kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kuwa na huduma za ziada za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja kwa kutumia biashara mtandao kusafirisha na kufanikisha usambazaji wa huduma na bidhaa za wateja kama vile uagizaji wa magari; vitabu na bidhaa nyingine kwa kushirikiana na kampuni kubwa duniani kama vile Alibaba, Amazon na eBay.

Imetolewa na ;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF