WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujenga hoja vizuri katika Bunge linalotarajia kuanza vikao vyake wiki ijayo mjini Dodoma, kwa kuwa wabunge wa vyama vya upinzani wameongezeka bungeni.
Hayo
yalisemwa jana Dar es Salaam na Pinda, baada ya kuaga mwili wa
aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere, aliyefariki akiwa
Maryland nchini Marekani akipatiwa matibabu.
Akizungumzia
Bunge la sasa, Pinda aliwashauri wabunge wanaounda Bunge hilo ambao
wengi wao ni vijana, kuzingatia maslahi ya taifa na sio itikadi za vyama
vyao na kuwasisitiza wabunge wa CCM, kujipanga na kwenda na hoja.
“Kila
upande ujiandae kwenye kuwasilisha hoja, kuna ongezeko la wabunge wa
upinzani, sasa wabunge wa CCM ni lazima nao wajipange na kujenga hoja
vizuri,” alisema Pinda.
Alisema kwa mtazamo wake, Bunge ni zuri na sio la mivutano kwa kuwa kila mmoja amejipanga kuwasilisha hoja zitakazomgusa mwananchi kwa lengo la kumsaidia.
Alisema kwa mtazamo wake, Bunge ni zuri na sio la mivutano kwa kuwa kila mmoja amejipanga kuwasilisha hoja zitakazomgusa mwananchi kwa lengo la kumsaidia.
Akizungumzia
utawala wa Awamu ya Tano wa Rais John Magufuli, Pinda alisema kila zama
zina kitabu chake; na kwa utawala wa Rais Magufuli ameanza vizuri na
kuomba Watanzania kumuunga mkono ili kufanikisha azma ya maendeleo ya
taifa.
Alisema
katika uongozi wake, ndio muda wa kuhakikisha Dira ya Taifa ya
Maendeleo inayoisha baada ya miaka 10 ijayo, inapaswa kuwa imetekelezwa,
hivyo hatua mbalimbali anazozifanya rais, ikiwa ni pamoja na kubana
matumizi, ni mambo muhimu.
“Hatua
zinazofanywa na Rais Magufuli ni za msingi katika kuhakikisha dira ya
Taifa ya Maendeleo inatekelezwa, ni vyema Watanzania wote tumuunge mkono
juhudi zake”, alisema Waziri Mkuu mstaafu Pinda.
No comments:
Post a Comment