Leo
tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki
silaha. Kwa mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba
wapo baadhi ya wamiliki wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki
silaha wanazozimiliki.
Kufutia
hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao
kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta
silaha ambazo hazijahikikiwa. Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na
silaha ambayo haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo
kupoteza sifa ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.
Tunatoa
agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha
hizo pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili
ya uhakiki.
Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi
No comments:
Post a Comment