RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIRKI DHIFA YA KITAIFA NA MGENI WAKE RAIS KAGAME - LEKULE

Breaking

3 Jul 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIRKI DHIFA YA KITAIFA NA MGENI WAKE RAIS KAGAME



Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akigonganisha bilauri na Mke wa Rais wa Rwanda, Mama Jeannette Kagame katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (katikati) Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akigonganisha bilauri na Rais wa Rwanda Paul Kagame, katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais Kagame.  Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam juzi usiku.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa amesima kutoa heshima wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais Kagame (kulia kwake). Kulia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Wa pili  kulia ni Mke wa Tanzania Mama Janet Magufuli na kushoto ni Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto), Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo (kulia).

Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) akizungumza na  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame aliyetembelea Tanzania kwa ziara ya Kikazi.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (kushoto) akiwa na Spika Mstaafu Anne Makinda (kulia), wakimsilikiza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) akizungumza na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Musa Salum (katikati).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwenye Dhifa Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaa kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (wa tatu kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam juzi usiku. Kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anayemfuatia ni Mke wa Rais wa Tanzania mama Janet Magufuli na wa pili kulia ni Mke Kagame, mama Jeannette Kagame.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza kwenye Dhifa Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaliwa na mwenyeji wake Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto). Kulia ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Janet Magufuli na wa pili kushoto ni Mke Kagame, mama Jeannette Kagame.

Baadhi ya waalikwa waliohudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame, Ikulu jijini Dar es Salaam juzi usiku, wakimsikiliza Rais Kagame (hayupo pichani).

Rais wa Rwanda Paul Kagame akimsalimia Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Katikati ni Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto) akimtambulisha Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimtambulisha Spika Mstaafu Anne Makinda kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwana mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame, wakiangalia burudani ya kikundi cha Matarumbeta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akimsindikiza Mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (wa pili kulia) baada ya kumalizika kwa Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi wakati wakiondoka kwenye ukumbi wa Ikulu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (katikati) wakati wakiondoka kwenye ukumbi wa Ikulu.Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba na kulia ni Mke wa Rais Mama Janet Magufuli.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO

No comments: