Rais wa
Afrika Kusini, Jacob Zuma, akijibu maswali mengi ya Wabunge na Maseneta
kuhusu kesi inayojulikana kama "Gupta" inayoibua maswali mengi katika
utawala wake.
Jumatau
hii Juni 27, Wizara ya Fedha ya Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama
Katiba ya Afrika Kusini imemuamuru Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
kulipa Dola 500,000 kama kitita cha pesa kiliyotumiwa kinyume cha sheria
katika kashfa ya makazi yake binafsi ya Kandla.
"Jumla ya
kitita ambacho Rais Zuma anapaswa kulipa ni sawa na Rand 7814555", sawa
na sehemu ya kazi iliyofanyika katika ujenzi wa makazi yake kwa
matumizi ya fedha za umma, mamlaka ya Hazina ya taifa imebaini kwenye
stakabadhi iliyokabidhiwa Mahakama ya Katiba.
Juma
lililopita Mahakama nchini Afrika Kusini ilitupilia mbali jaribio la
Rais Jackob Zuma, kukata rufaa kupinga hukumu iliyoagiza afunguliwe
mashtaka ya rushwa zaidi ya 800.
Rais Zuma
alijaribu kupindua uamuzi wa awali wa mahakama wa mwezi Aprili, ya
kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka ifungue upya mashtaka ya rushwa dhidi
yake, yaliyofutwa mwaka 2009, siku chache kabla ya kuwa Rais.
Mashtaka
dhidi ya Rais Zuma yanahusu rushwa, udanganyifu, utakatishaji fedha na
matumizi mabaya ya fedha za uma, kuhusu ununuzi wa silaha za kijeshi
uliogharimu mabilioni ya dola za Marekani.
Rais Zuma
amekuwa akipamabana kusafisha jina lake kutokana na tuhuma kadhaa za
rushwa zinazomkabili, sambamba na ukosolewaji mkubwa kuhusu sera ya
ajira nchini humo.
Mwaka
2009, ofisi ya mwendesha mashtaka ilitoa maelezo ya kwanini ilimuondolea
Rais Zuma mashtaka zaidi ya 700 ya rushwa, ikisema mawasiliano
yaliyonaswa wakati wa utawala wa rais Thabo Mbeki hayakuwa na uhusiano
wowote kwenye kesi ikiwa wangefungua mashtaka.
Uamuzi
huu wa ofisi ya mwendesha mashtaka, ulisafisha njia kwa Rais Zuma,
kiongozi wa chama tawala nchini humo cha ANC, kuwania urais wiki chache
baadae.
Mawasiliano yaliyorekodiwa ambayo yalifahamika kama "Spy tapes" yalifanywa kuwa siri, hadi pale yalipowekwa wazi mwaka 2014 baada ya muda mrefu wa ushindani wa kisheria mahakamani, kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance. RFI
Mawasiliano yaliyorekodiwa ambayo yalifahamika kama "Spy tapes" yalifanywa kuwa siri, hadi pale yalipowekwa wazi mwaka 2014 baada ya muda mrefu wa ushindani wa kisheria mahakamani, kesi iliyofunguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance. RFI
No comments:
Post a Comment