Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry
Kufuatia
kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa
mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo
wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi.
Msimamo
huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni kufuatia kura ya maoni ijumaa wiki
iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema hayo
katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond
Hata
hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo tofauti na
kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema
Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura
kujitoa.Lakini Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.
John
Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo ya
mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano ya
kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo.
Akizungumzia
kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na
Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana
kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia
kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa
dunia kwa ujumla. BBC
No comments:
Post a Comment