Mkuu
Wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi
(hawapo pichani) katika siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi
Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kulia ni Mkuu wa Kituo
cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji.
Mkuu
Wa Kituo cha Life and Hope Bagamoyo Sober House, Al-Kareem Bhanji aki
akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika kwenye siku ya
Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa
wa Pwani kushoto ni Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga.
Wananchi
wakifatilia mada mbalimbali kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita
Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
Waathirika wa Dawa za Kulevya akiandamana siku ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
Maandamano yakeendelea.
Kikundi cha Sana cha Bagamoyo wakiigiza kama Waathirika wa Dawa za Kulevya.
Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga akiwa kwenye picha ya Waathirika wa Dawa za Kulevya.
Mkuu Wa Kituo cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji akiwa kwenye picha ya Waathirika wa Dawa za Kulevya
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Kituo
cha Usaidizi Wa Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope
Bagamoyo Sober House leo,June 26,2016 kimeadhimisha siku ya Kimataifa ya
Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya.
Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka June 26 lakini kwa Mwaka huu Kituo cha Sober kimeadhimisha siku hiyo Wilayani Bagamoyo.
Akizungumza
katika Maadhimisho hayo,Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed
Mwanga amesema vita vya Mapambano ya Dawa za Kulevya si vya Serikali
pekee wala vya mtu mmoja bali ni vita vya kila mtu,ambaye anapaswa
kuwajibika katika eneo husika ili kutokomeza kabisa uingizwaji Wa Dawa
hizo.
Pia,Mkuu
huyo Wa Wilaya ametoa wito kwa Viongozi Wa Dini ,Wananchi pamoja na
Vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikiana kwa pamoja katika kutoa
taarifa za kuwafichua waingizaji Wa Dawa hizo ili Serikali kuwachukulia
hatua kali za kisheria.
Amesema,Serikali
imeahidi kupatikana kwa eneo kubwa ili kuendeleza kituo hicho na
kuwasaidia vijana ambao ndio waathirika wakubwa Wa janga hilo na kuitaka
jamii kuwatambua na kuwabaini waathirika wa Dawa hizo.
Kwa
upande wake,Mkuu Wa Kituo hicho cha Life and Hope Bagamoyo Sober
House,Al-Kareem Bhanji amesema kituo hicho kimesaidia watu zaidi ya 100
mpaka sasa,ambapo ametoa Changamoto za ukosefu wa Majengo kituoni hapo
jambo ambalo limepelekea kwa sasa kulipa kodi kubwa ya pango.
Pia
ameiomba Serikali kupatikana Ardhi ya kutosha ili kuweza kuongeza
majengo na kukidhi haja ya kupokea Waathirika 200 ikiwa Wanaume 150 na
Wanawake 50.
No comments:
Post a Comment