WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja.
Mbunge
wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa
kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha
na vitendo vya ushoga.
“Napenda
kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii
naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata
muongozo wako,” alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi
hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa
kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana
huyo anajutia kufanya vitendo hivyo.
Alisema
mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba
vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha
vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurahia kitendo kile, na
jambo la kusikitisha asubuhi hii (jana), mwendeshaji wa kipindi hicho
alialikwa katika kipindi cha asubuhi cha kituo hicho, badala ya kuomba
radhi ameishia kujitetea.
Kutokana
na maelezo hayo, aliomba Mwongozo wa Spika pamoja na Kanuni na kwa kuwa
serikali ipo, itoe kauli kama inaruhusu ushoga au kama hairuhusu ni
hatua gani inachukua kwa kituo hicho ili iwe fundisho kwa vingine.
Naye
Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Maro (CCM) alisema kijana huyo
aliyehojiwa na Kipindi cha Take One cha Clouds Tv amewaaibisha wakazi wa
Musoma mkoani Mara, hivyo aliiomba serikali imchukulie hatua kwa sababu
anaweza kuwafundisha tabia zisizofaa vijana wengine.
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akijibu miongozo hiyo, alisema jambo hilo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
==> Msikilize shoga huyo akihojiwa
No comments:
Post a Comment