Juni
26 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alitangaza kuteua Wakuu wa Wilaya
zote nchini, na Wakuu wa Mkoa watatu. Kati ya Wakuu wa Wilaya 139
walioteuliwa, 39 wamebakishwa katika nafasi zao huku 100 wakiwa ni
wapya.
Katika
hali ya kushangaza siku moja baada ya orodha hiyo kutangazwa, Rais
Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Ikungi iliyopo mkoani
Singida. Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Fikiri Avias Said ndani
ya masaa 24 tangu uteuzi wake.
Sababu
kuu ya Rais kutengua Uteuzi huu ameisema leo hii wakati wa hafla ya
kuwaapisha Wakuu wote walioteuliwa, ni kwamba jina lilikosewa, na kusema
kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi ni Bwana Miraji Mtaturu ambaye
ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza,
No comments:
Post a Comment