Ujenzi wa
majengo ya ghorofa yaliyo chini ya kiwango yaliripotiwa katika jiji la
Dar es salaam miaka ya nyuma iliyopita ambapo kariakoo kulikuwa na
ghorofa 64, taarifa nyingine ilikuwa ni ya jengo la ghorofa kuporomoka
na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
April 06 2016 Bodi ya Wakandarasi imemfikisha Mahakamani Kisutu Dar es salaam mfanyabiashara na Mwanasiasa Thomas Ngawaiya kwa kosa la kufanya shughuli za ujenzi wa jengo la hoteli lenye thamani ya zaidi ya MILIONI 500 Kinondoni Dar es salaam bila kutumia wakandarasi waliosajiliwa.
Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ambayo amedhaminiwa na wadhamini wawili ambapo masharti yake kila mmoja awe na ahadi ya MILIONI 250 na hati ya nyumba.
Akizungumza baada ya kesi hiyo Mwanasheria wa Bodi ya usajili wa makandarasi, Saddy Kambona amesema….>>>’Mtuhumiwa
ameshtakiwa kwa kutokutumia wakandarasi waliosajiliwa kama ambavyo
sheria ya bodi ya makandarasi namba 17 ya 1997 na ilipofanyiwa 2008
inavyotaka kwamba majengo yote ya matumizi ya umma lazima yajengwe
kitaalamu na wakandarasi waliosajiliwa kwa hiyo shughuli hizo za ujenzi
zimekuwa zikiendelea bila kuwepo kwa wakandarasi waliosajiliwa badala
yake umekuwa unafanywa na mafundi wa kawaida tu’.
No comments:
Post a Comment