TCRA waikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi - LEKULE

Breaking

1 Apr 2016

TCRA waikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi pamoja na Amos Shiyuka (kushoto) wakishuhudia.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya leseni.

Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.

Alisema kampuni hiyo inayoundwa na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake nchini Namibia.

Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu kibiashara.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kukabidhi leseni ya biashara kwa Kampuni ya Agano Safi itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services).
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa pande zote mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo.

Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka (kulia).
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. 

No comments: