PICHA ZA ZIARA YA NAPE MKOANI MARA NA SHINYANGA - LEKULE

Breaking

16 Apr 2016

PICHA ZA ZIARA YA NAPE MKOANI MARA NA SHINYANGA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0ei1qtyYx_rHSfdyQBqr7RkiGmC1SW5J46XWq_JEEsyZ3thyphenhyphenkgW_uQQGKYbJHFv4ZM6YECsX2xghzHPtUUO4p7AUPKOq1E1g0vIBzChjubP86uhmaJAvPS7uN-GayYAjpPnwYR_ceAGc/s1600/14.JPG
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na washika dau wa Habari, Utamaduni Sanaa na michezo wa mkoa wa Mara ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukutana na wadau hao wakiwemo watumishi wa serikali .

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye leo ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara na Shinyanga ambapo alikutana na Watumishi na wadau walio chini ya Wizara yake.

Waziri Nape alipokea taarifa zaSerikali pamoja na maoni ya wadau mbali mbali ambapo aliwapongeza kwa kuwa na maoni mazuri na kusisitiza Wizara yake itakuwa karibu nao na kufanya ziara za mara kwa mara katika kuhakikisha mambo waliyopanga yanafanikiwa.

Waziri Nape aligusia mambo mbali mbali ya msingi wakati akiongea na washika dau waliokuwa chini ya wizara yake na kusisitiza kuwa Madiwani wanaoshiriki katika mipango mji wanatakiwa kuzingatia kutenga viwanja vya michezo kwa watoto wa eneo husika pia alishauri mikoa kuanzisha vituo vya utamaduni wa mkoa ambavyo vitakuwa vyanzo vya kutunza utamaduni lakini pia sehemu ya kuvutia utalii akitolea mfano kituo cha Bujora mkoani Mwanza. 

Mhe. Nape pia aliwataka Makatibu Tawala za Mikoa wajenge utamaduni wa kukutana na vyama vya michezo kwani wao ni walezi muhimu wa vyama hivyo. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggx-orsbb95TXp-R-heBc547tJ6paHQeilcNL7InazEFfbd4qhqQ1tiZ_M_e9LkPZ9dXd9T9TFxtv_HrXl8WFrDkchchjqxuH8rnXYQmQggCrK1CrWQomJ2ioG_Ktt0COsWPIh2-NGGIo/s1600/5.JPG
Sehemu ya washika dau waliohudhuria kikao cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mara.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhB9ZTttWFgRb7lfANRMjHHz7aRgRJCP9yMfrmf30nBWJ7ge87a60H5fJa9AadJ9ASngeksTVbkhjHbBj45GtsvZ9wTePMp8h1kaeAYF_TSkdwB9S3cXiNOTUIEoo4Fa-P2IWZSfwMPdqY/s1600/4.JPG
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgv-B_3V8lOAVVcF41ttpg6DgN31ujdFTGgNUqEt7UVuwh7dsiO3Umg9azqa2FcPJ65G48e6XBTsMMGrXJLoUf6W2xUfkvMmlt4jrmS4qUxTrrO4YEv9Rzt3V9t8ibZSBl-9xzTQJKaQ74/s1600/5.JPG
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara ambapo aliwataka viongozi hao kutembea kifua mbele kwani ilani waliyoiandaa inatekelezwa vyema.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLBXW9Yvg0ovcud3DZyRRiNUd4lyn6oKEnmADyHuhhmRKDfdTLz6f_36AezljOKEXE44Pe8TxNvlVVJQKdG-1CAcsbvAlkIESHIACSHowBzJy6DuoFV3a-dTy1A8mUlD2lm9AwC-Ul4Fk/s1600/7.JPG
Sehemu ya uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMTTDXnDPnwf2E8wZpwu3L0c29Liub-0Shn_EIX9JpNKkY2P4JiSGh9-C7wGR16MzNw_KRlg824xmmRBPGyfEY3BFWh7rtg5lK3hSYMF6E_morhKiKIFeW_Jyznjv-ZvBqxCyaFvA5OLQ/s1600/13.JPG
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watumishi wa serikali pamoja na wadau wa sekta ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wa mkoa wa Shinyanga .

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments: