February 2016 iliripotiwa ripoti ya
kuzima injini ya Pantoni na kuleta tafrani kwa abiria, sasa ni takribani
miezi miwili tangu tukio hilo litokee. Daraja la Nyerere ‘Kigamboni’
lililozinduliwa jana limeonekana msaada mkubwa kwa wakazi wa Dar es
salaam hasa Kigamboni.
Usiku wa siku ambayo Daraja lilizinduliwa April 19 2016 imetolewa taarifa ya gari moja aina Toyota Hiace yenye namba za usajili T271 CRG kuserereka
kutoka kwenye pantoni na kuzama baharini. Pantoni hilo lilikuwa
likivuka kutoka Posta kuelekea Kigamboni Alfajiri ya April 20 2016.
Watu waliosadikiwa kuwa ndani ya gari
hilo ni wawili au watatu na mpaka sasa mtu mmoja ameokolewa na Jeshi la
zimamoto na uokoaji. Kati ya watu walikuwamo ndani ya gari hilo ni dada
wa Brown Mwakalago ambaye ameyazungumza haya……
>>>tulikuwa
tunatoka msibani Mbeya, yule dada yangu aliyekuwa mle ndani ya gari
alikuwa amepanda kwa sababu alikuwa anajisikia vibaya, tulipokuwa
tumekaa pembeni tukaona gari linaserereka kwenda mbele na kwenda kwenye
maji kwa hiyo dada yangu hajaonekana mpaka sasa hivi’
Pia Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita amefika na kulizungumzia kuwa ….>>>’uwenda
zile lock za kule nyuma hawakuzifunga, huenda ni uzembe kwa hiyo
tunangojea ripoti huko ndani tujue nini kilichojiri jana usiku’
kiongozi wa uokoaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Abdu Swala amesema …….>>>‘tulifanikiwa
kutoa mwili mmoja na bado tunaendelea kutafuta chombo chenyewe na mtu
ambayo inasemekana walikuwemo watu wawili hadi watatu taarifa kamili
bado hazijatolewa’
No comments:
Post a Comment