NAIBU WAZIRI WA HABARI AKIWA BAGAMOYO CHUO CHA TASUBA - LEKULE

Breaking

6 Apr 2016

NAIBU WAZIRI WA HABARI AKIWA BAGAMOYO CHUO CHA TASUBA

 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba)  Bw. Michael Kadinde wa kwanza kushoto akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura kulia wakati wa ziara ya Mh. ya Mheshimiwa Waziri aliyoifanya katika Taasisi hiyo iliyopo Bagamoyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili. (Picha na Benjamin Sawe- WHUSM).
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura kulia akiangalia moja ya tuzo ya ubora iliyopewa taasisi hiyo Afrika Mashariki wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri aliyoifanya katika Taasisi hiyo iliyopo Bagamoyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili.Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa  TaSUba  Bw. Michael Kadinde
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura kulia akimuuliza jambo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba)  Bw. Michael Kadinde kushoto wakati wa ziara aliyoifanya katika taasisi hiyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba)  Bw. Michael Kadinde wa kwanza kushoto akimuonyesha Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura kulia ramani mpya ya taasisi hiyo wakati wa ziara aliyoifanya katika taasisi hiyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili.
 Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo Mwalimu John Mponda akionyesha umahiri wa kucheza ngoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura hayupo pichani wakati wa ziara aliyoifanya katika taasisi hiyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba)  Bw. Michael Kadinde wa kwanza kushoto akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi  katikati moja ya sanaa iliyotengenezwa na wanafunzi wa taasisi hiyo wakati wa ziara aliyoifanya Mh. Wambura katika taasisi hiyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili, wa kwanza kulia ni Afisa Mipango wa taasisi hiyo Bw. Emanuel Bwire.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura katikati akionyesha zawadi aliyopewa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba) wakati wa ziara  aliyoifanya Mh. Wambura katika taasisi hiyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazowakabili, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Nuru Khalfan Mrisho.

: Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura wa pili kutoka kulia akiongea na watumishi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba) hawapo pichani wakati wa ziara aliyoifanya katika taasisi hiyo kujionea utendaji kazi na changamoto zinazoikabili taasisi hiyo, wa kwanza kulia ni  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Nuru Khalfan Mrisho.  (Picha na Benjamin Sawe- WHUSM). 

No comments: