Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi akifungua mafunzo ya
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma yalioandaliwa na Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji
Mstaafu Salome Kaganda.
Kamishna
wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome
Kaganda akitoa maelezo mafupi yanayohusu Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na
Taasisi za Umma leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Mhandisi John William Kijazi.
Baadhi
ya Washiriki wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
waliohudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Washiriki wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
waliohudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi (hayupo pichani) leo jijini
Dar es salaam.
Baadhi
ya Washiriki wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
waliohudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi akiongea na Waandishi
wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na
Taasisi za Umma yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma leo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO).
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi amewaasa Wakuu wa
Mashirika na Taasisi za Umma kuzingatia Maadili ya Viongozi wa Umma
katika kutekeleza makujumu yao.
Katibu
Mkuu alisema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa akifungua mafunzo
ya viongozi hao yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma ili kuhakikisha wanaendana Uongozi wa Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli.
“Maadili
yana umuhimu wake mkubwa katika utawala wa maendeleo ya nchi, kupitia
maadili mema wananchi wanajenga imani na viongozi pamoja na Serikali yao
kwa ujumla” alisema Balozi Mhandisi Kijazi.
Ili
kuhakikisha mafunzo yanakuwa yenye tija, Balozi Mhandisi Kijazi
amewasisitiza viongozi hao kutumia muda vizuri na kujikumbusha na
kujifunza maadili hayo kwa manufaa ya mashirika na taasisi zao pamoja na
taifa kwa ujumla.
Balozi
Mhandisi Kijazi alitaja umuhimu wa maadili katika jamii na kusema kuwa
yanasaidia kusimamia rasilimali za umma na kuzitumia kwa maslahi ya
wote, kuongeza tija na thamani ya huduma, zinazotolewa na Serikali,
kudhibiti mianya ya ukiukwaji wa maadili na vitendo vya rushwa, kujenga
ujasiri wa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma.
Maadili
pia yanasaidia wananchi, viongozi na Watumishi wa Umma kutoa mchango wa
haraka katika kutekeleza maendeleo ya nchi, kuepuka utata wa maamuzi ya
migongano ya kimaslahi, kuwavutia wawekezaji, kujenga na kudumisha
amani na utulivu pamoja na kuondoa na kukomesha ubinafsi kwa viongozi.
Aidha,
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi amesema kuwa ukiukwaji wa maadili
unaathari hasi kwa taifa ambapo alizitaja baadhi ya athari hizo kuwa ni
rasilimali za nchi kunufaisha wachache, wananchi kukosa haki zao za
msingi kutokana na rushwa na upendeleo, viongozi wa umma kujilimbikizia
mali isivyostahili bila kujali hali za wananchi wanaowaongoza, kupungua
kasi ya uwekezaji pamoja na kudhohofika kwa uchumi wa nchi.
Madhara
mengine ya kutojali maadili ni wananchi kukosa imani na Serikali yao,
kuchochea vurugu pamoja na wananchi kutotii sheria za nchi na hivyo
kuhatarisha usalama, amani na utulivu wa nchi.
Kwa
upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Jaji Mstaafu Salome Kaganda alipokuwa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi
amesema kuwa misingi ya maadili na maadili yanalenga katika kuzuia
mgongano wa maslahi, upendeleo, matumizi mabaya ya rasilimali za umma na
taarifa za ofisi na mwenendo usiofaa kwa viongozi wa umma ili
kuimarisha na kuendeleza dhana za uadilifu, uwajibikaji na uwazi ambazo
ni sifa muhimu za kiongozi.
Ili
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, Jaji Mstaafu Kaganda amesema
kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa
watumishi ambapo kuna zaidi ya viongozi 15,000 huku Sekretarieti ina
wafanyakazi 200 nchi nzima.
Mafunzo
hayo yamehudhuriwa na washiriki 40 ambapo yalifanyika kwa Mawaziri,
Manaibu Waziri, Mkatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Wenza wa Viongozi,
Wakuu wa Mikoa.
No comments:
Post a Comment