Mbunge
wa Kigoma Kaskazini na Kiongozi wa ACT-WAZALENDO Mhe Zitto Kabwe
akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New York,
Marekani, jana. Mhe Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao
waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge
la jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia
upinzani, pia yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo
wake juu ya kasi ya rais wa wamu ya 5. Zitto ni mmoja ya vijana kwenye
Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na
uwezo wa kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na
kuitikisa serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye
ndiyo alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea
wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala. Na
pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa
ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank
na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na
kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard
University huko Boston. MA.
Picha na Vijimambo Blog New York
Picha na Vijimambo Blog New York
Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi.
Zitto
akitafakari swali kabla kujibu, Zitto aliulizwa kama yupo tayari
kuungana na Ukawa na kama yupo tayari kungombea kiti cha urais kupitia
chama chake ACT, majibu yalikuwa yupo tayari kuungana na ukawa lakini
anaitaji kujua nini faida ya kuungana na kama kuungana ili kuing'oa CCM
basi iwe na nguvu kweli kweli na ifanikiwe kwani asinge penda kuungana
na nakubakia msindikizaji tu bila faida endelevu na kama yupo tayari
kugombea kiti cha urais basi atafanya hivyo akiwa amesha jiandaa
vilivyo ili akigombea apata ushindi wa kishimdo na kuing'oa CCM na siyo
vinginevyo.
Mkurugenzi
wa Ford Foundation Rakesh Rajani akiuliza swali kwa Zitto. Bw. Rajani,
ambaye pia ni mwansilishi wa taasisi za HakiElimu na TWAWEZA, ndiye
aliyeandaa mkutano huo.
Shabani Mseba akiuliza swali kwa Zitto swali lake nini mipango ya maendeleo jimboni kwake.
Na
jibu lake lilikuwa mipango yake ni kuhakikisha elimu inakuwa na
mwamko ndani ya mkoa wake. Kwani elimu imeshuka sana na ufaulu wa watoto
umezidi kuwa chini.
No comments:
Post a Comment