Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokelewa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin, wakati wa hafla ya kuzindua
Mtandao mpya wa Teknolojia ya kisasa wa 4G hapo katika viwanja vya
Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Michenzani
Mjini Zanzibar. Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi Zanzibar Balozi Ali Abeid Aman Karume na kulia ni Waziri wa
Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Balozi Ali Karume kwenye hafla ya uzinduzi wa mtandao Zantel wa 4G.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana Benoit
Janin akiteta na Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo kwenye hafla
hiyo fupi.
Warembo
wa Kampuni ya Zantel wakifuatilia tukio la uzinduzi wa mtandao wa 4G
kwenye simu zao za mikononi zitakazowawezesha kupata huduma mbali mbali
ikiwemo kuonanan na yule watakayempigia.
Balozi
Seif akipokea zawadi maalum kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu
za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin mara baada ya kuzindua
mtandao wa 4G wa Kampuni hiyo.Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Balozi Ali Abeid Amaan Karume.
Picha no:-808 ni:- Balozi Seif Wa Tatu kutoka Kushoto akiwa katika picha
ya pamoja na uongozi wa Zantel, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi na wageni wengine walioalikwa kwenye uzinduzi wa Mtandao wa 4G.
Kulia
ya Balozi Seif ni Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Katibu Mkuu wake
Dr. Juma Malik na kushoto ya Balozi ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Zantel Tanzania Bwana Benoit Janin, Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit
Kombo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipando Nd. Khamis Mussa Pamoja na
Afisa muandamizi wa Kampuni ya Zantel hapa Zanzibar Ndugu Baucha.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Viongozi na
Watendaji wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel wanapaswa kuongeza
kasi ya utendaji ili waendelee kuwa watoa huduma bora hapa Nchini licha
ya kasoro ndogo ndogo zinazoweza kurekebishwa kwa wakati muwafaka.
Alisema
Zantel kwa kipindi cha miaka Minane mfululizo imekuwa ikitunukiwa
zawadi ya mlipa kodi bora katika kundi la walipa kodi wakubwa, zawadi
ambayo hutolewa kila mwaka na Mamlaka ya Kodi Tanzania { TRA }.
Balozi
Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma
mpya ya mtandao wenye kasi zaidi wa G Nne { 4G } kwa upande wa Zanzibar
iliyofanyika katika Bustani ya Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar hapo Michenzani Mjini Zanzibar.
Alisema
ushindi huo ni fahari kubwa kwa Zantel pamoja na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar yenye hisa zake ambayo ilipata changamoto kubwa na hatimae
kufanikiwa kupata kibali cha kuanzishwa kwa Kampuni hiyo mwaka 1999.
Balozi
Seif alieleza kwamba kodi zinazolipwa na Zantel zilizofikia zaidi ya
shilingi Bilioni 18 kwa mwaka 2015 pekee zinasaidia Taifa katika kuweka
urari wa nakisi ya Bajeti yake.
Hata
hivyo Balozi Seif alitanabahisha kwamba yapo matatizo yanayolalamikiwa
na Wananchi kuhusu kukatika kwa mawasiliano kwa baadhi ya wakati jambo
ambalo huleta usumbufu unaochangia baadhi ya wanandoa kutoaminiana.
Mapema
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Tanzania Bwana
Benoit Janin alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umekusudia kuimarisha zaidi
huduma zake ili kuhakikisha unapatikana mtandao wa kasi utakaorahisisha
ukuaji wa teknolojia hapa Zanzibar.
Alisema
matumizi ya teknolojia hiyo mpya ya mtandao wenye kasi zaidi wa G Nne {
4G } utasaidia watumiaji kupata huduma zenye ubora na uhakika pamoja
na kuwepo kwa ongezeko la kasi la matumizi ya mtandao kama vile huduma
za skype, You Tube na mitandao mengine ya Kijamii.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/4/2016.
No comments:
Post a Comment