Hatimaye wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.
Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao jana Jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo.
Katika ripoti hizo zilizowasilishwa, Mkoa wa Mwanza unaongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na mkoa wa Arusha 270.
Mkoa wa Dar Es Salaam.
Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.
“Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73, ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwa nini unakuwa na watumishi hewa wachache, nataka kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina,”alisema Makonda .
Mkoa wa Arusha.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda alisema mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,
Mkoa wa Dodoma.
Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana alisema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo una watumishi hewa 101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali milioni 287.3 kwa kipindi cha miezi sita.
Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha ya hao, kuna watumishi 145 ambao hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huenda idadi ya watumishi hewa ikaongezeka.
Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal Mstaafu Salum Kijuu alisema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1
Mkoa wa Katavi.
Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael Muhuga alisema mkuo huo umegundulika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia hasara serikali Milioni 20.7.
Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral Mstaafu Emmanuel Maganga alisema katika mkuo huo wamebaini kuwepo watumishi hewa 171ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.
Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa huo,Merck Sadick alisema wamebaini mkoa wake unawatumishi hewa 111 ambao wameisababishia serikali hasara ya milini 281.4.
Mkoa wa Lindi
Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi alisema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.
Mkoa wa Manyara.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa huo,Joel Bendera, alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Milioni milioni 313.9.
Mkoa wa Mara.
Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa huo,Magesa Mulongo alisema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi hewa 94 ambao wameitia hasara serikali milioni 121.
Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Mkuo huo,Amos Makalla alisema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi hewa 98 ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.
Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven Kebwe,ambapo alisema mkoa wake umegundulika kuwepo na watumishi hewa 122 ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.
Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa mkoa huo, Halima Dendegu amesema mkoa wake umebainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea, ambapo watumishi hao 17 wameitia hasara serikali milioni 216.5.
Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa John Mongella alisema mkoa wake umengundulika kuwa na watumishi hewa 334.
Mkoa wa Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Dkt Rehema Nchimbi alisema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.
Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku akishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.
Mkua wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu Zerote Steven alisema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia hasara serikali milioni 55.6.
Mkuo wa Ruvuma,
Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.
Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka alisema mkoa huo umegundulika kuwa na watumishi hewa 62 ambao wameitia hasara serikali ya Milioni 320.9.
Mkoa wa Singida,
Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew Mtigumwe alisema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake ni 231 na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.
Mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alianisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa ni 48 ambapo wanaitia hasara Serikali Milioni 118.7.
Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104 ambapo alisema kuwa tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.
Hata hivyo katika mkoa wa Shinyanga hali ilikuwa tofauti na mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi hewa kutokana na mikakati iliyowekwa kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.
Pia, Mkoa wa Songwe hauna watumishi hewa kunatokana na kwamba mkoa huo ni mpya na mkuu wake wa mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.
No comments:
Post a Comment