Ugiriki
Kamishna wa Jumuiya ya Ulaya wa maswala ya wahamiaji amesema kuwa Ugiriki imefurika na wakimbizi na wahamiaji.
Dimitris
Avramopolous ametoa wito kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo ya Ulaya
kusaidia katika kusuluhisha hali hiyo badala ya kuiachia Ugiriki au
Italia pekee.
Kati ya wahamiaji 2003 wanakisiwa kuingia Ugiriki kila siku.
Wengi wao hawawezi kusonga mbele kwa sababu ya vikwazo vikali vilivyowekwa na Austria na mataifa ya Balkan.
Wahamiaji wanaoingia Ugiriki
Mwandishi
wa BBC anasema kuwa matamshi ya Bwana Avromopolous ni ishara kuwa
kiongozi huyo wa wahamiaji katika Jumuiya hana nia ya taifa lake
kuzuiliwa kuwa mwanachama wa muungano wa paspoti wa Schengen.
Kwa
kawaida mtu ye yote aliye na paspoti ya Schengen ana uhuru wa kusafiri
bila vikwazo kwa mataifa mengine wanachama wa muungano huo
No comments:
Post a Comment