Papa Francis alaani mauaji ya watawa Yemen - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 6 March 2016

Papa Francis alaani mauaji ya watawa YemenPapa Francis amelaani mauaji ya watu 16, wakiwemo watawa wanne wa Kikatoliki, mauaji yanayoshukiwa kufanywa na wapiganaji Waislamu, katika nyumba ya wazee nchini Yemen hapo jana.
Vatikan imesema, Papa ameshtushwa na kusikitishwa sana na vifo hivyo, ambavyo vilielezewa kuwa kitendo cha uovu.
Ripoti za awali zilieleza kuwa watawa hao wanne walitoka India, lakini shirika moja la Vatikan, baadae lilisema watawa hao kati yao wawili walikuwa kutoka Rwanda, Mkenya mmoja na mmoja kutoka India.
Hakuna kundi lilodai kufanya mauaji hayo katika mji wa Aden, wenye bandari.
Post a Comment