Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump' - LEKULE

Breaking

27 Mar 2016

Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'

Raia wa Mexico wanaosherehea sikukuu ya pasaka wamekuwa wakichoma sanamu za mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Republicans Donald Trump.
Mojawapo ya tukio hilo la kushangaza limefanyika katika kitongoji kimoja cha wakaazi walio na kipato cha chini kiitwacho La Merced.
Wakaazi wengi wa La Merced wamejitokeza kushuhudia kuchomwa kwa kikaragosi cha Trump badala ya kile cha yule mfuasi wa Yesu Kristu aliyemsalito Judas Iscariot.
Image captionWamexico wengi hawampendi bw Trump tangu alipotoa matamshi ya kuwakejeli wamexico.
Wamexico wengi hawampendi bw Trump tangu alipotoa matamshi ya kuwakejeli wamexico.
Desturi hiyo ya kuchoma vikaragosi hutumiwa na wamexico kuelezea hisia zao dhidi ya wanasiasa wenye sera wasizozipenda wakitolea mfano wa jinsi Judas Iscariot, alivyomsaliti Yesu.

No comments: