Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani katika chama cha Democtrats bwana Bernie Sanders ameshinda majimbo mengine mawili katika jitihada za kuongeza hesabu zake katika kampeni za kuwania tikiti ya chama cha democtrats dhidi ya mpinzani wake anaongoza mbio hizo kwa sasa Bi Hillary Clinton.
Miongoni mwa majimbo aliyoshinda Bwana Sanders ni Washington State - na vilevile Alaska.
Hata hivyo licha ya ushindi huo Bw Sanders bado ana kibarua kigumu cha kumfikia au hata kumpiku Bi Clinton ambae tayari anaungwa mkono na wajumbe 1,700 na sasa anahitaji wajumbe wengine 700 tu kushinda tiketi hiyo ya chama chake .
Matokeo ya kura ya awali katika jimbo la Hawaii yangali yanasubiriwa.
Naye anaeongoza kinyanganyiro cha kuwania tiketi ya chama cha Republican , Donald Trump, amesema sera yake ya mambo ya nje ni 'Marekani kwanza'.
Katika mahojiano na gazeti la New York Times amesema nia yake sio kwamba anataka Marekani iwe pekepeke duniani, bali ana wasiwasi na kile anachosema ni kupunjwa kwa taifa hilo lenye uwezo mkubwa duniani na wengi wa washirika wake .
Amesema anataka Marekani iache kuendelea kununua mafuta kutoka Saudia hadi pale waSaudi wakubali kupeleka majeshi kupigana na wanamgambo wa IS.
Ameongeza kusema kuwa akishinda urais atayaondoa majeshi ya Marekani kutoka Japan na Korea Kusini kama mataifa hayo hayatailipa zaidi Marekani.
No comments:
Post a Comment