Baada ya mvutano wa muda mrefu wa Simba kufuatilia fedha zake za usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi kutoka katika klabu ya Etoile du Sahel, kitu ambacho kilipelekea Simba kuishitaki Etoile kwa FIFA, Sasa majibu yanatajwa kupatikana.
Simba ilikuwa inaidai Etoile dola 300,000/= ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania lakini pia imelipwa dola 19000/= kama fidia ya usumbufu wa kufuatilia deni hilo, Rais wa zamani wa Simba Aden Rage ambaye alikuwa akituhumiwa kula hela hizo, ameeleza mambo kadhaa.
Rage amesema kwanza majibu yamepatikana kwa wanaosema nilikula hela za Okwi, ila ushauri ni kuwa hizo fedha za Okwi zinaweza kuisaidia klabu kujenga uwanja wake wa mazoezi na nyumba za wachezaji kwa ajili ya kambi. Lakini Rais wa sasa wa SimbaEvans Aveva alipoulizwa alisema hajui kama fedha hizo zimefika, ila kwa sasa wanafikiria Ligi.
Simba ilimuuza Emmanuel Okwi kwenda klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2013 kwa dau la kihistoria la dola 300000/= lakini baaadae Okwi aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo na kuamua kurudi kwao Uganda kuendeleza maisha yake ya soka. Kwa sasa Okwi anacheza soka la kulipwa Sønderjysk ya Denmar
k
k
No comments:
Post a Comment