Moja ya
stori zilizochukua headline usiku wa March 13 2016 ni pamoja na hii ya
ajali ya basi la Leina Tours lililoanguka maeneo ya Kimara Bucha, Dar es
salaam na taarifa zake zikitolewa tofauti na baadhi ya watu.
Leo March 14 2016 Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amelitolea ufafanuzi sahihi na kusema>>
‘Jana
tarehe 13/3/2016 majira ya saa 3 na robo usiku, gari lenye namba T 878
CAH Scania Bus lilikuwa linatoka Kahama na kuja Dar es salaam, wakati
likiwa kwenye barabara ya Dart mbele yake kulikuwa na gari aina ya Rav4
likija uso kwa uso’
‘Wakati
analikwepa bahati mbaya gari likamshinda na dereva kwahiyo akaenda
kugongana na costa ya abiria, katika ajali hiyo tumewapoteza watu wawili
akiwemo dereva wa basi lililokuwa likitoka Kahama pamoja na abiria
mmoja’
‘Lakini
madereva wa magari mawili, Rav 4 na costa hadi sasa hawajapatikana,
taarifa tulizonazo ni kwamba wale majeruhi wengine hadi sasa bado
wanaendelea vizuri na tunawaombea waweze kupona ’
No comments:
Post a Comment