TAKUKURU Yaanza Kuchunguza Jinsi Waziri Lukuvi alivyokataa Rushwa ya Bilioni 5


Takukuru imeanza kuchunguza taarifa kwamba Waziri wa Ardhi, William Lukuvi alikataa kupokea rushwa ya Sh5 bilioni iliyotaka kutolewa na wafanyabiashara wawili wakubwa ili kuwapitishia mradi wa Sh84 bilioni.

Katika mahojiano  na gazeti  la Mwananchi  hivi  karibuni, Waziri Lukuvi alisema kwamba lengo la wafanyabiashara hao ilikuwa ni kufanikisha mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwa bei kubwa kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.

Licha ya kukataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao, Lukuvi alisema mtandao huo wa wafanyabiashara ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza rushwa.

Jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kutokana na taarifa ya kiongozi huyo, ofisi yake iliamua kuchukua chanzo hicho na kuanza kazi ya uchunguzi.

Hata hivyo, Mlowola hakutaka kuweka wazi kazi ya uchunguzi huo imeanza lini wala ilipofikia. 

 “Kueleza tumeanza lini hilo ni suala la kiufundi, tumeshaanza kushughulikia,” alisema Mlowola ambaye Rais John Magufuli amemuidhinisha rasmi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo baada ya kukaimu kwa miezi kadhaa.

Katika ufafanuzi wake, kamishna huyo wa zamani na mkurugenzi wa Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi, alisema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa ikichukua tuhuma yoyote ya rushwa kutoka chanzo chochote baada ya kuripotiwa.

Katika mahojiano hayo, Waziri Lukuvi alisema wafanyabiashara hao waliwaeleza marafiki zake wa karibu kuwa wangempa rushwa.

Mji huo mpya wa Kigamboni unajumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila na eneo lote hilo lina ukubwa wa takribani ekari 6,000.

Awali mradi huo ulitarajiwa kugharimu Sh13 trilioni ambazo zingetolewa na Serikali, lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi ili kuujenga na Serikali ishughulikie uwezeshaji wa awali.

Lukuvi ambaye alihamishiwa Wizara ya Ardhi mapema mwaka jana na kubakizwa katika wizara hiyo na Rais Magufuli, alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa wizara.

“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja ni wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe Sh5 bilioni ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi,” alisema Lukuvi.

Aliongeza: “Wakati naingia tu wizara hii nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili walipata taarifa wakaja mbio kutaka kuniona.”

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wafanyabiashara hao walitaka walipwe Sh141 milioni kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa Sh5 milioni kwa ekari, jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa Sh5 milioni, kisha Serikali tumlipe Sh141 milioni kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa.

"Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji.

Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya Sh84 bilioni kuwalipa wawekezaji hao hewa kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.

“Niliwaambia Serikali haiwezi kuwalipa fedha hizo na badala yake waende kuiendeleza ardhi wenyewe kulingana na mradi unavyotaka. Walitaka kutajirika kwa ujanja ujanja,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“Eti walidai wamekopa fedha benki kwa ajili ya mradi huo. Haiingii akilini mtu utumie Sh5 milioni, halafu uje uvune mabilioni ya fedha kwa kuvuka pantoni tu.”
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF