ALIKIBA NA SAUTI SOL WAUMALIZA UTATA WA KOLABO - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 13 March 2016

ALIKIBA NA SAUTI SOL WAUMALIZA UTATA WA KOLABOBaada ya kundi linaloundwa na vijana wanne wenye uwezo mkubwa wa kuimba kutoka nchini Kenya maarufu kama Sauti Sol kuachia wimbo wa Uncondinationally Bae walioshirikiana na msanii nyota kutoka Tanzania maarufu kama Alikiba, umepokelewa vyema na mashabiki wao huku kukiwa na maswali juu ya ngoma hiyo.ALIKIBA AND SAUTI SOL NEW

Sauti Sol ndio walikuwa wakwanza kupost kupitia mitandao ya kijamii hususani Instagram na Youtube juu ya wimbo huo ambapo awali ulikuwa ukisomeka Sauti Sol FT Alikiba jambo ambalo lilizua utata kwa mashabiki kwa kuwa na sintofahamu juu ya nyimbo hiyo huku wakijiuliza hiyo ni nyimbo ya pamoja au Alikiba ndiye aliyeshirikishwa.12751033_550143455147954_1821844788_n(1)

Jambo lililozidi kuwatia hofu mashabiki wa msanii Alikiba ni kutoona post yeyote ya msanii huyo kuhusu ngoma hiyo mpya, jambo ambalo siyo kawaida yake pale anapokuwa ametoa ngoma mpya alikiba and sauti sol 11

Kwa kuzingatia hayo mtembezi.com ilipiga story na moja ya watu wa karibu na Alikiba na akaueleza mtandao huu kuwa hiyo ngoma ni ya pamoja siyo kwamba Alikiba kashirikishwa hivyo watakapo badilisha ndio wataanza kuiunga mkono kazi hiyo.alikiba and sauti sol

Mtembezi iliendelea kusubiria kitakachojiri huku ikiendelea na pitapita yake mtandaoni na kukutana na Post ya Alikiba iliyorekebishwa na kuandikwa Sauti Sol and Alikiba tofauti na awali ilikuwa inaonesha kuwa yeye ndiye aliye shirikishwa, halikadhalika kwa upande wa Sauti Sol nao wamebadilisha.10576233_1051166311609647_1834885204_n


Haya sasa Kenya, zamu yetu!! Tanzania let’s go!!!!#UnconditionallyBae with my brothers@sautisol x officialalikiba#SautiSolAlikiba #LetsUnite Link in bio ameandika Alikiba kupitia ukurasa wake wa Instagram.alikiba sauti sol

Post a Comment