Mtakumbuka
kwamba leo ni siku ya 15 ya utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa la
kuwataka kuwaondoa kwenye malipo watumishi hewa.
Natumia fursa hii kutoa taarifa kwa Umma kuwa Agizo hilo limetekelezwa kama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza.
Taarifa za watumishi hewa tayari zimewasilishwa kwa maandishi Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuanzia mwishoni mwa wiki.
Kwa
sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi na zitakapokuwa tayari kwa matumizi
ya Umma zitatolewa kwa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuufahamisha Umma.
Hivi sasa taarifa hizi zinakusanywa kwa pamoja ili kupata idadi kamili.
Wakati
huo huo, napenda kuufahamisha Umma kuwa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es
Salaam (DART) yameanza kufanya mazoezi ya utoaji huduma toka siku ya
alhamisi tarehe 24/03/2016. Tunategemea wiki hii mtoa huduma ataendelea
kuongeza idadi ya mabasi ya kufanya mazoezi kabla zoezi hili halijaanza
rasmi.
Imetolewa:
George B. Simbachawene (Mb)
Waziri wa Nchi
29/03/2016.
No comments:
Post a Comment