MAJIBU YAMETOLEWA: Mabasi ya haraka yakianza kazi Dar zile Daladala barabara ya pembeni vipi? - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 29 March 2016

MAJIBU YAMETOLEWA: Mabasi ya haraka yakianza kazi Dar zile Daladala barabara ya pembeni vipi?


Mabasi ya mwendo wa haraka kwenye jiji la Dar es salaam yapo kwenye majaribio ya kuanza kazi hivi karibuni na inawezekana ulijiuliza kama itakuwa ni chaguo lako upande Mabasi hayo au daladala barabara ya pembeni, yaani kutakua na daladala zinazofanya kazi kwenda na kutoka town japokuwa mabasi ya haraka yameanza kazi?
Taarifa ikufikie kwamba mabasi hayo yatakapoanza daladala zote zitatoka na alielithibitisha hilo March 29 2016 ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)  David Mziray wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukosekana vituo kwenye barabara ya Morogoro.
>>>’huu mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapoanza mabasi ya daladala yote yatatoka,  ndio maana utaona mabasi mengi yanayotumia barabara hizi za mchanganganyiko kwa maana magari ya kawaida na mabasi, hakuna vituo vya daladala kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito, yakishaanza haya mabasi ya mwendo wa haraka, huduma hizi za mabasi ya kawaida zitasimama’
David Mziray pia ameeleza taarifa ya kukamatwa kwa magari zaidi ya 100 ndani ya siku nne kutokana na kuvunja sheria ikiwemo kupandisha gharama za nauli za daladala na ukatishaji wa safari >>> ‘Kati ya hayo magari 105, 36 yameshafikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka na kuweza kujibu tuhuma wanazokabiliwa na wakibainika wana makosa kutakuwa na faini, kupelekwa jela au vyote viwili’

Post a Comment