Siku ya March 11 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
alifanya ziara ya kutembelea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya
Kinondoni kujionea kero za uharibifu wa miundombinu ikiwepo barabara na
kuamua kutoa agizo kwa Manispaa ya hiyo kuhakikisha inafanya ukarabati wa maeneo yaliyoharibika ndani ya siku 14 kabla ya kuwawajibisha.
Leo March 25 ripota wa millardayo.com
aliongozana na mkuu huyo wa mkoa katika mitaa tofauti ikiwa ni pamoja
na barabara ya Mwananyamala ili kujionea hatua zilizofikiwa na kukuta
ukarabati ukiendelea…
Lakini bado mkuu wa mkoa hakuonyesha kuridhishwa na kazi iliyokuwa ikiendelea na kusema>> ‘Nilitoa
siku 14 ukarabati wa hii barabara uwe umekamilika, nashukuru leo
nimepita na nimekuta kazi imeanza, lakini nimewataka wahusika waangalie
uwezekano wa kuwa na barabara za kudumu kwa muda mrefu‘ ;-Paul Makonda
‘Kuna
barabara pale Makumbusho wamejenga alafu wameharibu mitaro, sasa
nimemtaka mkandalasi arudi haraka na arekebishe, maana wamejaza mchanga
kwenye mitaro, hatuwezi kuwa na barabara zisizokuwa na mitaro, baada ya
siku kumi nitarudi tena kuhakikisha kama wamekamilisha‘ ;-Paul Makonda
No comments:
Post a Comment