Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA Dkt.Agness Kijazi (Katikati)
akitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi
machi hadi mwezi Mei, 2016. Kushoto ni Samwel Mbuya ambae ni Meneja
Kitengo Kikuu cha Habari TMA Dar es salaam na Kulia ni Dkt.Hamza Kabelwa
ambae ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mamla ka
ya Hali ya Hewa nchini TMA imewatahadharisha Wananchi pamoja na Taasisi
mbalimbali ikiwemo za Uokoaji, kujiandaa juu ya namna ya kukabiriana na
athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika ambazo tayari
zimeanza kunyesha hapa nchini.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi alitoa tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.
Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
Alisema
Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo
mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo
mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi zikajiandaa
kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Mkutano
baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA
ilikuwa ikitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi
cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.

No comments:
Post a Comment