Askari wawaili wa kulinda amani kutoka Tanzania wakipiga doria nje ya mji wa Goma, Oktoba 6, 2013.
Nani
alihusika na mauaji ya askari wa kulinda amani wa Tanzania mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 5, 2015? Tukio hilo bado linaibua
maswali mengi hadi sasa, kwani ushahidi wa kwanza wa uchunguzi
ulioendeshwa na mahakama ya kijeshi ya Congo unatofautiana na matokeo ya
hivi karibuni ya wataalam wa Umoja wa Mataifa.
Wataalam
hao wanabaini katika ripoti ya siri, kwamba majeshi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (FARDC)yalihusika katika shambulio hilo la kuvizia
dhidi ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO0 katika eneo
la Beni. Mara tu baada ya ushahidi huo, mamlaka ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo ilianzisha uchunguzi. Jumamosi hii, Machi 5, RFI
inaonyesha ushahidi wa kwanza wa ripoti ya mahakama ya kijeshi ambayo
inabaini kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na waasi wa Uganda wa
ADF-Nalu na kwamba askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC)
waliwasili kwenye eneo la tukio baada ya hali hiyo kutokea.
Mahakama
ya jeshi katika eneo la Beniiliwahoji watu watao, wakiwemo maafisa wanne
waliotumwa katika wilaya ya Beni wakati wa tukio hilo, na mtu mmoja
aliyenusurika katika shambulio hilo, muendesha pikipiki ya kukodiwa.
Mashahidi
hao watano, wote walikanusha ripoti ya timu ya wataalam wa Umoja wa
Mataifa. Mkuu wa bataliani ya kwanza mjini Mayi Moya, karibu na eneo la
shambulio, alikuwa Oicha na alisema alipokea simu akiambiwa kwamba mji
wa Beni umeshambuliwa. Anasema kuwa alichukua pikipiki akiambatana na
mlinzi wakewakielekea katika eneo la tukio. Kutokana na milio mingi ya
risasi na baada ya kubadilishana risasi na kundi la wahalifu, aliamua
kwenda kutafuta msaada.
Kwa
mujibu wa ripoti hii ya utafiti na ushahidi uliotolewa, wanajeshi wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasadikiwa kuwa waliwasili katika
eneo la shambulio baada ya mapigano na inasadikiwa kuwa waligundua miili
miwili ya askari wa kulinda kutoka Tanzania na raia watatu. Pia
waliokota silaha zilioachwa naaskari wa Tanzania, ambazo walizkabidhi
kwa wahusika baadaye, ripoti hiyo inaeleza.
Shahidi
raia aliohojiwa, yeye, anaeleza kuwa alikuwa nyuma ya msafara wa
wanajeshi wa Tanzania wakati shambulio hilo lilitokea. Raia huyo
aliiambia mahakama ya kijeshi ya Congo kwa shambulio hilo liliendeshwa
na raia wenye silaha, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, ambao
ripoti ya mahakama ya kijeshi inabainisha kuwa ni waasi wa Uganda wa
ADF-Nalu.
Mwendesha
mashitaka kwenye mahakama ya kijeshi pia amesema kuwa alikutana na
mwakilishi wa timu ya mtaalam wa Umoja wa Mataifa. Inasemekana, kupitia
ripoti hii, kwamba wataalam wa Umoja wa Mataifa pia wana mashahidi
watano ambao wanathibitisha toleo lao kuhusu tukio hilo, Mashahidi hao
wa wataalam wa Umoj aw aMatiafa ni mpiganaji wa ADF-Nalu, afisa wa jeshi
la congo (FARDC).
No comments:
Post a Comment