March 23 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na Baraza la Wazee wa Dar es salaam na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika jamii.
Katika
kutatua changamoto zinazowakabili wazee, Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeonyesha imedhamiria kutoa kipaumbele
kwa wazee na imesisitiza kusimamia Sera ya Serikali ya kutoa huduma za
afya bure kwa wazee. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu amezungumza na waandishi wa habari na kusema….
>>’kuhusu
huduma kwa wazee hasa matibabu tunataka kuwathibishia bado inabaki kuwa
ni sera ya Serikali na kwamba wazee Tanzania wanatakiwa kupata
matibabu bure, kuanzia gharama ya kumuona Daktari, vipimo na Dawa.
Naendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatekeleza
Sera ya Serikali ya kutoa huduma za afya bure ikiwemo kuanzisha dirisha
la wazee‘.
>>>’na
kuonyesha kwamba nimedhamiria nimeshaongea na watu wa bima ya afya
mwezi ujao tutatoa matangazo ambayo tutaweka katika vituo vyote vya
Serikali ‘Mzee kwanza, Mzee alikuwa kama wewe na wewe utakuwa kama yeye,
tafadhali toa kipaumbele cha huduma kwa wazee’ tayari tumeshaaanza
tunatafuta siku ya kuyazindua ili kuendelea kuhamasisha kipaumbele kwa
wazee‘
No comments:
Post a Comment