Jeshi la Polisi Dar lilivyozikusanya Mil 577 za wakosaji Barabaran - LEKULE

Breaking

18 Mar 2016

Jeshi la Polisi Dar lilivyozikusanya Mil 577 za wakosaji Barabaran


Polisi Kanda maalum Dar es salaam kupitia kitengo cha usalama barabarani wametoa taarifa ya makosa ya barabarani kuanzia March 07 2016 hadi March 18 2016 kuwa wamefanikiwa kukamata magari mbalimbali kwa makosa ya usalama barabarani na jumla ya Tsh Milioni 577.8  zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa muda wa siku 11.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema…..>>>madereva wametakiwa kuwa waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka  adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku’
Aidha hapo awali Kamishna Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro alitoa taarifa ya kukamata madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo moja katika eneo la Mbezi beach ambapo Jeshi la polisi linamshikilia pia mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Benson Muro Charlesmwenye umri wa miaka 32.

No comments: