Ibrahimovic: Klabu za Uingereza zinanitaka - LEKULE

Breaking

28 Mar 2016

Ibrahimovic: Klabu za Uingereza zinanitaka

PSGMshambuliaji matata wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic amesema klabu kadha za Ligi Kuu ya Uingereza zinamtaka.

Kwa sasa anachezea mabingwa wa ligi ya Ufaransa Paris St-Germain.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, ambaye mkataba wake katika klabu hiyo ya Ufaransa utamalizika mwisho wa msimu huu, amehusishwa na kuhamia Manchester United, Chelsea na Arsenal.
"Nimekuwa ninatafutwa lakini hebu tusubiri tuone hili litafika wapi,” amesema. “Lakini itahitaji kuwa kama harusi, lazima kila pande zitake sana kuwa pamoja.”
Ibrahimovic ameshinda ligi katika nchi nne tofauti Ulaya.
Alishinda akiwa Uholanzi (Ajax), Italia (Inter Milan, AC Milan), Uhispania (Barcelona) na Ufaransa (PSG).Baada ya kusaidia PSG kulaza Troyes 9-0 mapema mwezi huu, Ibrahimovic alisema: “Kwa sasa (mambo yalivyo ni kwamba), sitakuwa PSG msimu ujao. Bado nina mwezi mmoja unusu wa kukaa hapa.
"Wakibadilisha mnara wa Eiffel na badala yake waweke sanamu yangu, basi nitakaa.”
Ibrahimovic amefungia taifa lake mabao 62 katika mechi 111.

No comments: