Ndugu zangu,
Jirani zetu Waganda wanakwenda kupiga kura Alhimisi Februari 18, 2016. Naziona ishara za Yoweri Museveni kushinda uchaguzi huo.
Kwanini?
Nina
bahati ya kufuatilia kwa karibu siasa za Uganda tangu pale vikosi vya
Tanzania vilipoingia Kampala na kumwondoa madarakani Idd Amin.
Kwenye
Serikali za mpito akaja Profesa Kilonge Lule aliyedumu Ikulu kwa siku
68. Akaapishwa Godfrey Binaisa mwaka ule ule wa 1979. Ukafanyika
uchaguzi wa kwanza wa ' maruweruwe' wa 1980 uliomwingiza madarakani Dr
Milton Obote.
Mwelekeo
mbaya wa Uganda ulionekana kwenye mkutano wa Moshi, Tanzania, mwaka
1979. Ni pale Waganda walipokutanishwa na Julius Nyerere wajadili
mustakabali wao kwenye ardhi ya Tanzania. Museveni alikuwepo, Dr. Milton
Obote alizuiwa na Nyerere asije Moshi akitokea uhamishoni Lusaka.
Sababu? Nyerere alifahamu, kwenye mkutano huo uwepo wa Obote ungeharibu
zaidi kuliko kujenga. Nyerere alimwambia Obote aandike tu barua ya
kuutakia heri mkutano!
Uchaguzi
wa ' Maruweruwe' wa 1980 ulimwingiza madarakani Obote ukawa mwanzo wa
mapambano mapya ya Waganda. Waasi sasa waliongozwa na Yoweri Museveni.
Museveni
akaunda NRA- National Resistance Army. Alikuwa na uzoefu wa vita vya
msituni. Akaingia madarakani 1986. Miaka kumi baadae nilifika Kampala na
kutembea hata maeneo ya vijijini. Niliona jinsi Museveni na NRM-
Nationali Resistance Movement alivyofanikiwa kuiga mfumo wa TANU na CCM
katika kutengeneza mtandao vijijini.
Tatizo la
upinzani Uganda ni kama kwengineko Afrika. Umegawanyika sana na
wanaogombania wametokana kwenye mfumo huo huo wanaopingana nao. Mfano,
Amama Mbabazi kwa Waganda wengi wanamwona kama ' mkosaji tu'.
Aliutumikia mfumo wa Museveni kwa miaka mingi hadi pale aliponyimwa
nafasi ya kugombea urais kutoka chama chake.
Kuna mengi ya kuyachambua. Nitarudi tena...
No comments:
Post a Comment