Uongozi
wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90
kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, lazima hospitali hiyo
itafungwa.
Kauli
hiyo imetolewa jana jioni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza
na viongozi Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na na Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.
Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla akikagua mahabara ya hospitali hiyo ambayo
alikutana na matatizo mbalimbali ikiwemo mashine na vifaa kutotumika
ipasavyo na kuagiza uongozi wa kufanya maboresho ndani ya miezi mitatu
huku akiahidi kuifungia endapo itashindwa kutekeleza maagizo hayo.
Dkt.
Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali,
vituo vya afya na zahati ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio
waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali.
Miongoni
mwa maagizo hayo ni uboreshaji wa huduma kwa kuwepo na vifaa tiba na vya
maabara za kisasa, dawa za kutosha, kuaanza malipo ya mtandao.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri huyo alibaini kwamba hospitali hiyo haina
baadhi ya vifaa vya maabara, ambavyo ni muhimu kwa uchunguzi wa magonjwa
mbalimbali, ikiwemo mashine ya CT-Scan na kuwepo kwa vifaa vibovu
ambayo havijafanyiwa matengenezo, ukiwemo mfumo mbovu wa ukusanyaji taka
ngumu na nyepesi.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akiangalia moja ya maeneo ya wodi hizo
ambapo alikuta hali ya uchafu pamoja na kuwa na mpangilio mbovu wa namna
ya utoaji wa huduma.(P.T)
“Sijaridhishwa
na uendeshaji wa hospitali hii na utoaji wa huduma
zinazotolewaa ninakuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, John Luanda kurekebisha
mapungufu yaliyopo baada ya miezi mitatu nitarudi nikikuta huduma bado
hairidhishi nitakifunga kituo.,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Aliongeza kuwa akikuta huduma hadhirishi atafunga hospitali hiyo licha ya kuwa ya Serikali, hivyo hatasubiri kutumbuliwa jipu.
Dk.
Kigwangalla akitoa maelezo kwa Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa
Njombe-Kibena, Dk. Samwel Mgema wakati wa maagizo hayo ndani ya siku 90
na endapo hawatafanya utekelezaji ataichukuia hatua ya kuifungia.
Dkt.
Kigwangalla aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mpango kazi na
mkakati wa kuboresha mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo na
kuuwasilisha kwake.
Aliutaka uongozi wa hospitali huo kujenga chumba cha upasuaji cha wakina mama na watoto.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe, Mgema alisema watatekeleza maagizo hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akielekea kwenye baadhi ya majengo ya hospitali hiyo wakati wa ukaguzi huo.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akikagua eneo la kutolea huduma ikiwemo
wagonjwa wanaoingia kumuonna Daktari.
No comments:
Post a Comment