Watumishi sita wa sekta ya afya wasimamishwa kwa ubadhirifu wa milioni 145 - LEKULE

Breaking

29 Feb 2016

Watumishi sita wa sekta ya afya wasimamishwa kwa ubadhirifu wa milioni 145


IMG_3589
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Christopher Ngubiagai amewasimamisha kazi kwa muda usiojulikana watumishi sita wa idara ya afya akiwemo Maimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Timoth Sumbe, kwa tuhuma ya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 145 za mfuko wa afya ya jamii (CHF).
Wengine waliosimamishwa kazi ni aliyekuwa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Dk. Japhet Simeo ambaye  kwa sasa amehamia Tandahimba.
Pia wamesimamishwa kazi Katibu wa Afya Wilaya ya Iramba, Kalebi Ngughu, Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Sylveri Maganza, Katibu wa afya Alphonce na Katibu mwingine wa afya, Grace Maganga.
Akitoa tamko hilo zito mbele ya kamati ya ulinzi ya wilaya ya Iramba na waandishi wa habari, Ngubiagai alisema ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba, Halima Mpita ambaye amehamishiwa Tunduma akamatwe na kuletwa Iramba, ili kujibu tuhuma ya ubadhirifu huo wa fedha za umma.
“Nimewasimamisha kazi wafanyakazi hawa, ili kupisha uchunguzi wa kina uweze kufanyika na ikithibitika wanahusika na upotevu huo wa fedha CHF na `on call allowance` hatua za ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma zichukue sehemu yake,” alisisitiza.
Akifafanua, Ngubigai ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, alisema kati ya fedha hizo, shilingi milioni 64 ni gawio lililotolewa na  mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) kutokana na ada zilizolipwa na wanachama wa CHF wilaya ya Mkalama.
“NHIF ilitos  fedha hizo Julai mosi,  2013 kipindi wilaya ya Iramba ilijumuisha na jimbo la Iramba mashariki kwa wakati huo ambalo lilipata hadhi na kuwa wilaya ya Mkalama na uchunguzi wa awali unaonyesha fedha hizo hazikuingizwa kwenye akaunti yoyote zimeishia hewani,” alisema DC huyo kwa masikitiko.
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 600w" alt="IMG_3585" width="697" height="522" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />
Kaimu mkuu wa wilaya ya Iramba na mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida,akitoa taarifa ya kusimamisha watumishi wa idara ya afya kwa tuhuma ya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi 145 milioni za mfuko wa afya ya jamii (CHF) na za posho za watumishi wa afya (on call allowance),kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha),Pia ilikuwepo kamati ulinzi na usalama ya wilaya ya Iramba. (Picha na Nathaniel Limu.)
Aidha, alisema shilingi 81,180,000 za ‘on call alowance’, nazo hazikulipwa kwa walengwa na badala yake zimetumika kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Kaimu mkuu huyo ya wilaya alisema kuwa halmashauri ya Mkalama inafanya kazi ya ziada kudai fedha hizo kwa barua kumbukumbu MDC/A.10/3/27 ya 14/4/2014, MDC/  A.10/3/7 YA Julai 15/ 2014 na MDC/A.10/3/8 ya 15/2/2016, zote hazikuzaa matunda na hazijajibiwa hadi sasa.
“Kuna kila dalili kwamba wapo viongozi wa ngazi za juu ambao wameongoza kwa nyakati tofauti wameshiriki katika ‘dili’ hili chafu la kutumia fedha za umma kwa maslahi yao binafsi,hatutawaacha,tutawafuata huko waliko kuwakamata,ili kuja kujibu tuhuma hii,” alisema.
Ngubiagai ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wa umma wa wilaya ya Iramba na Mkalama kwenda sambamba na mapinduzi ya sasa ya kiutendaji ya “Hapa kazi tu”, na kuacha vitendo vya ubarudhilifu wa mali ya Umma ikiwemo rasilimali fedha kwa madai vitawaharibia maisha yao.
Na Nathaniel Limu, Iramba

No comments: