Vurugu Kubwa Zaibuka Wakati wa Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam - LEKULE

Breaking

27 Feb 2016

Vurugu Kubwa Zaibuka Wakati wa Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam


VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa  tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo katika ukumbi wa Karimjee  jijini Dar es salaam mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi  kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani.

Jambo hilo liliwachukiza   madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia.

Wakati UKAWA  wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo  wenyewe ,Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini,jambo lilowachukiza tena na kuibua patashika ndani ya ukumbi.




No comments: