Farasi huweza kubaini kati ya mtu aliye na furaha na aliye kasirika kwa kuangalia uso wa mwanadumu,utafiti umesema.
Katika
jaribio, kwa kutumia picha za mwanamume wanasayansi kutoka chuo kikuu
cha Sussex walionyesha kwamba farasi wanaofugwa nyumbani huchukizwa na
sura zilizokasirika.Wanasayansi hao wanasema kuwa ufugaji huo huenda umewawezesha farasi kuelewa tabia za binaadamu.
Matokeo hayo yamechapishwa katika jarida la Biology Letters.
Kundi hilo lilifanya vipimo vyake kwa kuwasilisha picha nyingi mbele ya farasi 28.
''Mtu mmoja anashikilia farasi huku mwengine akishikilia picha,''alielezea mtafiti Amy Smith.
Matokeo yake ,alielezea ni kwamba waliangalia picha za watu waliokasirika na jicho lao la kushoto.
Akili za wanyama zimeumbwa kana kwamba hisia zinazotolewa na jicho la kushoto huangaziwa na eneo la kulia la ubongo ambalo hutumiwa kuangazia hisia mbaya.
Watafiti hao pia waliweka vipimo vya moyo katika moyo wa farasi hao ,ambavyo vilibaini kwamba nyuso zilizokasirika hufanya myoyo ya wanyama hao kudunda kwa haraka.
Matokeo kama hayo yameripotiwa miongoni mwa mbwa na kuzua maswali kuhusu ni vipi kuishi na binaadamu kuna badili tabia za wanyama hao.
No comments:
Post a Comment